fbpx

Chaneli za ndani zaanza kurushwa bure

0

Sambaza

Hatimae kuanzia leo,chaneli za ndani zimeanza kuoneshwa bure kwenye visimbuzi vya kampuni za Ting, Starmedia, Continental na Digitek.

Teknokona kupitia kisimbuzi cha StarTimes imeshuhudia kuanza kuonyeshwa kwa chaneli hizo bila ya malipo yoyote kufanyika.

Hatua hiyo imekuja baada ya  kikao kilichofanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, wadau pamoja na wamiliki wa televisheni nchini.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema kupitia kikao hicho kwamba walikubaliana kuanzia Septemba 5 mwaka huu visimbusi vitaanza kuonyesha channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.

Ving’amuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV havitaonesha channeli za ndani kwa sababu leseni zao walizoomba na kupewa haziwaruhusu kuonesha chaneli hizo.

chaneli za ndani

Moya ya ving’amuzi maarufu nchini Tanzania.

Kurejea kwa matangazo ya chaneli za ndani itakuwa ni faraja kwa wateja wengi waliokuwa wakilalamikia mamlaka ya mawasiliano TCRA kwamba wanalazimika kuzilipia ili kona jambo ambalo halikuwa sahihi.

INAYOHUSIANA  Mkazo kuhusu kutolipia chaneli za ndani

Chaneli ambazo zinatakazoonekana bure kwa muda wote na mteja hatalazimika kulipia ili kuziona ni TBC1, ITV, Channel 10, Clouds TV, Star TV na EATV.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.