Simu zinazidi kuadilika ila kuna kitu kimoja bado kinasumbua wengi, nacho ni uwezo wa betri. Juzi juzi tumeandika kuhusu watafiti wa Chuo cha Stanford nchini Marekani katika ugunduzi wao wa teknolojia ya betri inayoweza kutengeneza mabetri bora zaidi na sasa inasemekana Google pia kupitia kitengo chao cha Google X lab nao pia wamejikita katika uchunguzi wa teknolojia ya betri bora zaidi.
Google tayari wanajikita pia kwenye teknolojia ya vifaa mbalimbali kama kwa ajili ya eneo la vifaa vya hospitalini, magari ya kujiendesha n.k na hivyo wanategemea ugunduzi wa teknolojia bora zaidi ya mabetri itasaidia sana katika maeneo hayo.
Google X lab ni moja ya kitengo muhimu zaidi ndani ya Google kinachohusika na utafiti na utengenezaji wa teknolojia za kitofauti na za kisasa zaidi.
Inasemekana kuna timu ya watu wanne ndani ya Google X lab ambao kazi yao pekee ni suala la teknolojia ya betri tuu. Timu inaongozwa na Bwana Ramesh Bhardwaj ambaye alikuwa kwenye kitengo cha betri katika kampuni ya Apple. Timu imekuwa imejikita katika eneo la betri tokea mwaka 2012, na inajikita zaidi katika kupata teknolojia ya kufanya mabetri yawe madogo zaidi lakini yenye uwezo mkubwa zaidi – hii inamaanisha kuchajika kwa haraka na kuwezo kukaa kwa muda mrefu zaidi.
Teknolojia ya mabetri bora ni muhimu kwa Google ambao wanategemea soko la simu janja kwa ajili ya Android, na pia wamejikita katika kutengeneza magari yanayojiendesha ambayo yanatumia umeme wa betri za kuchaji. Hivi vyote vinaitaji mabetri yaliyobora zaidi.
Hadi sasa bado haijajulikana timu hiyo imefikia wapi katika kazi zao ila ni jambo la kuvutia kutambua ya kwamba Google pia wamewekeza katika eneo hili muhimu sana kwa vifaa vya kisasa vya elektroniki.
Endelea kutembelea TeknoKona, mtandao wako namba moja wa habari za teknolojia Tanzania!
Soma Pia – Betri Inayojaa ndani ya Sekunde 60!
No Comment! Be the first one.