Unamiliki tableti inayokubali WiFi tuu na si kuweka laini, mtaani kwako hauna jinsi ya kupata WiFI, au kuna ugumu wowote umetokea kiasi ya kwamba huwezi kupata WiFi, je utawekaje apps kwenye tableti yako? Hii ni moja ya sababu ila kuna sababu nyingine mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu atake kuweka apps kwenye simu za android bila kutumia Google Play.
Leo TeknoKona tutakuonesha jinsi ya kufanya hivyo, iwe kwenye simu au tableti yako yoyote unayotumia programu endeshaji ya Android njia hii itakusaidia kuingiza/kupakua apps bila kupitia soko la Google Play.
Angalia sababu nilizoziandika apa chini kama moja wapo au zote zinaendana na sababu inayokuzuia kupata app unayoitaji. Naelewa simu nyingi za Android zilizopo sokoni kwa nchi zetu nyingi zikiwa kutoka kwa makampuni yasiyo na jina kubwa sana unaweza kukuta hazijaja na soko la apps la Google Play na hivyo ukajikuta unakosa apps mbalimbali.
Je kwa nini utumie njia hii?
- Wenye simu/tableti za Android ila hawawezi kupata huduma ya intaneti kwenye vifaa hivyo
- Unalo solo la Google Play Store ila hauna akaunti ya Google/Gmail inayokuwezesha kuingia kwenye soko hilo
- Unapata intaneti kwenye kifaa chako ila hauna app ya Google Play
- App unayoihitaji imeondolewa kwenye soko la Google Play kwa sababu yeyote ile
- App unayoihitaji Google wameona haina sifa ya kuwa kwenye simu/tableti yako na hivyo ukienda kwenye Google Play unaikosa app hiyo ingawa kwa uhalisia inaweza kufanya kazi kwenye kifaa chako
- App unayoitaka inapatikana kwa ajili ya watumiaji wa nchi flani tuu na hivyo kwa Tanzania au kwingine kokote haipatikani kwenye Google Play
- Au kwa sababu nyingine yeyote…
Njia itakusaidia kupakua apps za Android kwenye simu au tableti yako….;
- Bila kuwa na Google Play kwenye kifaa chako
- Ata kama kifaa hicho hakina intaneti
- Ata kama ujaweka akaunti ya Google kwenye simu/tableti yako
Vitu vya Kufahamu:
Kama vile programu za kompyuta za Windows zinaishia na .EXE basi jina rasmi la apps za Android ni .APK, kirefu cha APK ni Android Package File. Hivyo katika njia hii tutakukufundisha jinsi ya kupakua mafaili ya APK kwenye simu au tableti yako.
Hatua ya Kwanza: Ruhusu Uwekwaji wa Apps Kutoka Sehemu Zisizo Rasmi
Kupitia mipangilio yake (settings), programu endeshaji ya Android huwa hairuhusu apps kujipakua kwenye simu/tableti zake bila kupitia soko spesheli mfano Google Play. Kuruhusu jambo hili nenda kwenye sehemu ya ’Settings’ ya simu yako, kisha ‘Security’ halafu bofya kutiki eneo la ‘Unknown Sources’. Itakuuliza kama unahakika na unachokifanya, bofya Ok.
Settings > Security> Wezesha ‘Unknown Sources
Pia kama chini ya eneo hili la ‘Unknown Sources’ utaona sehemu imeandikwa ‘Verify Apps’, na inatiki ondoa tiki hiyo. Kama sehemu hiyo haipo basi tuendelee na hatua ya pili.
(Hakikisha mara zote baada ya kumaliza kupakua app yako unarudi hapa na kuondoa ‘tick’, patakulinda dhidi ya apps zitakazotaka kujipakulia apps zisizosalama.)
Hatua ya Pili: Shusha Faili la App ya Android (APK) unalolitaka Kutoka Kwenye Intaneti
Apps zote ata kwenye Google Play unapokuwa unaipakua huwa inakuja kwenye mfumo wa APK, mfumo huu kama tulivyouelezea hapo juu ndio jinsi mafaili ya apps ya Android hufadhiwa. Kwa kuwa atutatumia Google Play, basi itabidi utafute faili hilo sehemu nyingine na hii inaweza ikawa kupitia kivinjari kama cha Opera, Chrome au Firefox cha simu/tableti hiyo hiyo au nyingine au ata kwenye vivinjari vya kwenye kompyuta.
Kuna mitandao mingi sana ambayo unaweza kupata mafaili ya APK yaliyo salama kabisa kwa ajili ya apps mbalimbali. Njia rahisi ni kwenda Google na kuandika ‘JINA LA APP UNAYOTAFUTA’ halafu unaongezea ‘APK file’, mfano kama unataka kupakua app ya WhatsApp basi nenda Google na andika ‘WhatsApp APK file’ kisha bofya kutafuta.
Sehemu za Kupata APK
-Mtandao muhimu sana kwa usalama ni http://apps.evozi.com/apk-downloader/ . Kupitia mtandao huu wewe unaenda kwenye soko la Google Play kwenye kompyuta yako, bofya eneo la ‘linki’ pale juu, ikopi na uiweke kwenye eneo la kutafuta kwenye huo mtandao wa EVOZI, ukifanya bofya ‘Generate Download Link’ basi wao watakupatia faili la APK la app hiyo mara moja kutoka Google Play na utalishusha (download kwenye kompyuta yako.
– Mitandao mingine inayokuwezesha kupata mafaili ya APK kwa urahisi ni pamoja na http://www.crackapk.com/, http://play.mob.org/ http://www.androidapksfree.com/ http://globalapk.com/ na mingine mingi . Baadhi ya mitandao hii inatoa hadi apps zinazouzwa Google Play bure kabisa (Ila hatukushauri utafute apps hizo 🙂 Kazi kwako!)
Hatua ya Tatu: Hamisha Faili Lako la APK kwenye Simu/tableti unapotaka Kuiweka
Kama umeshusha faili la APK kupitia kivinjari cha simu/tableti yenyewe basi hatua hii haiitajiki, ila kama umeshusha faili hilo kupitia kompyuta basi itabidi kupitia ‘memori kadi’ au kwa kuchomeka waya wa USB basi uhamishe faili hilo kutoka kwenye kompyuta na kuliweka kwenye simu au tableti hiyo.
Hatua ya Mwisho: Bofya Faili Hilo la APK Kulipakua Kwenye simu au tableti yako
Kwa kutumia app ya kusoma mafaili yaliyokwenye simu/tableti yako, basi nenda kwenye sehemu ulipoweka faili hilo la APK na ulibofye kulifungua. Kama umelishusha (download) kwa kutumia kivinjari cha simu/tableti hiyo basi bofya tuu eneo la ‘notifications’ utakapoambiwa limemaliza kushushwa kwa asilimia 100.
Ukilibofya faili hilo la APK litafunguka kama hapa chini; Bofya ‘Install’, kisha tulia na subiri, itachukua sekunde chache tuu faili hilo kujipakua kwenye kifaa chako na katika kujipakua huku intaneti haitahitajika kabisa. UMEFANIKIWA!!!!
Njia hii inaweza kukusaidia ata kama pale ambapo una vifaa viwili vya Android, kwani badala ya kushusha app hiyo sehemu zote mbili kitofauti tofauti na hivyo kutumia bando yako kwa mara mbili zaidi basi njia hii itakusaidia kwani utalishusha faili mara moja tuu na kuweza kulitumia kuweka app hiyo kwenye vifaa vyako vyote.
No Comment! Be the first one.