fbpx

TCRA na sakata la kuonyesha chaneli za ndani

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Sakata la kuonyesha chaneli za ndani bila ya wateja kulipia limefikia sehemu ambayo mpaka serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa neno.

Dk Harrison Mwakyembe (Waziri) ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kutoa mwongozo utakaowezesha kampuni zilizokiuka masharti kuweza kurejea kuonyesha ya chaneli za ndani kama ilivyokuwa hapo awali.

Kampuni zilipewa leseni ya kuonyesha chaneli za kulipia lakini zikaingilia soko la wenzao kinyume cha utaratibu wa leseni zao. Inaelekea hawa wenzetu wanapenda kurusha haya maudhui ya chaneli za ndani, hivyo TCRA itoe mwongozo wa  nini wafanye ili kuendelea kutoa huduma~Dk. Mwakyembe.

kuonyesha chaneli za ndani

Dk Mwakyembe amesisitiza kuwa kampuni hizo zilivunja masharti ya leseni zao lakini Serikali iliwavumilia kwa kuheshimu utawala wa sheria.

Ni wazi kuwa kampuni zinazozungumziwa zimevutiwa na soko la kurusha chaneli za ndani basi wasifanye mbinu za chini chini badala yake wafuate utaratibu.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu imepotea tuma IMEI kwenda cop@vsl.net - Hii habari ni ya uongo, usifanye hivyo
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.