Google ni moja kati ya kampuni kubwa za kiteknolojia ya kimataifa iliyopo Marekani iliyobobea katika utoaji wa huduma na bidhaa za Mtandaoni. Kampuni hii imekuwa ikitoa huduma zake kupitia majukwaa yake mbalimbali ikiwemo Google search engine na Youtube.
Huduma zinazotolewa na Google ni nyingi na zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Huduma kwa wote, Huduma za kibiashara na Huduma za watengenezaji. Katika huduma hizi kuna ambazo zinapatikana ndani ya majukwaa tofauti tofauti na zingine zinajitegemea zenyewe.
Huduma kwa wote: Unapokuwa na akaunti ya Google unakuwa umeunganishwa moja kwa moja na baadhi ya huduma zao zinazopatikana kupitia majukwaa yao. Majukwaa hayo ni pamoja na Google Play, Google Workspace, Gmail na Youtube. Kupitia jukwaa la Google Play store utaweza kupakua programu mbalimbali unazoweza kutumia katika simu janja yako, Kupitia jukwaa la Google Workspace utakutana na huduma za kiofisi kama Google Docs, Google Sheets na Google slides. Jukwaa la Youtube litakuwezesha kuangalia na kutuma video mtandaoni.
Huduma za Kibiashara: Google kupitia majukwaa yake mbalimbali inatoa huduma zinazosaidia biashara kukua na kutambulika mtandaoni. Majukwaa hayo ni pamoja na Google my Business, Google Analytics na Google Ad Manager. Kupitia jukwaa la Google my Business utaweza kutengeneza akaunti ya Google kwaajili ya biashara yako itakayowezesha wateja kukupata mtandaoni na kwenye ramani ya Google Maps. Kupitia jukwaa la Google Analytics utaweza kuona taarifa mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya biashara yako mtandaoni. Pia kupitia jukwaa la Google Ad Manager utaweza kutengeneza matangazo kuhusu biashara yako na kuruhusu matangazo katika tovuti yako yatakayokuingizia hela.
Huduma za Watengenezaji: Kupitia majukwaa mbalimbali Google hutoa huduma zao kwa watengenezaji wa programu za Android, iOS pamoja na Tovuti. Majukwaa hayo ni pamoja na Firebase, Google Cloud na Flutter. Jukwaa la Firebase linasaidia watengenezaji wa programu kutengeneza na kuziendesha programu zao kupitia huduma mbalimbali zilizopo kwenye jukwa hilo. Jukwaa la Google Cloud linasaidia watengenezaji pamoja na wamiliki wa biashara kusimamia biashara zao mtandaoni. Flutter ni lugha inayotumika na watengenezaji kutengenezea programu mbalimbali zinazotumika kwenye simu na kompyuta.
No Comment! Be the first one.