Ukiachana na umaarufu wake, bado Gmail ndio huduma ya kutuma na kupokea barua pepe ambayo inatumiwa sana duniani. Ukiachana na kutuma na kupokea barua pepe tuu kuna mambo mengi ambayo unaweza ukafanya kwa kutumia Gmail.
Kila huduma ili kuwa bora lazima upate zaidi ya kile ambacho unategemea si ndio? Sasa basi Gmail ina manjonjo kibao tuu ambayo pengine kwa namna moja au nyingine ndio yanaufanya mtandao huo kuendelea kukua siku na siku.
Tuyafahamu Mambo Yenyewe
- Tafsiri Email Zinazokuja Kwa Lugha Zingine
Unaweza ukapokea barua pepe (email) ambayo inakuja katika lugha nyingine, kwa mfano inaweza ikawa kichina. Hili likitokea kupitia Google kuna sehemu ya “View translated message” kwa juu ya barua pepe hiyo na kisha unaweza ingia na kuchagua “Translate message” na hapo Google wenyewe watafsiri barua pepe hiyo kwenda katika kiingereza. …. fikiri umepokea email ambayo imetumwa kwa kichina mfano 🙄

- Fanya Roboti Likusadie Kuandika Barua Pepe
Ndio inawezekana sana na siku hizi hii teknolojia wanaiita ‘artificial intelligence’, hii inamaanisha kuwa unaweza ukawa unaandika barua pepe lakini ukashangaa roboti akawa na uwezo wa kuotea neno linalofuatia au hata kumalizia maneno kabisa wakati unayaandika.
Na pia hili haliishi hapo hapo tuu pia huduma hii ina uwezo wa kukisia majibu ambayo unaweza toa katika barua pepe uliyopokea. hii kwa kiasi kikubwa inasaidai kuokoa muda katika kuchapa barua pepe ya majibu.

- Fanya Barua Pepe Kuwa Na Usiri Na Pia Kupotea Baada Ya Muda Fulani
Hivi unajua unaweza kutuma barua pepe kupitia Gmail na ukaiamuru ifutike baada ya muada fulani? ndio inawezekana kabisa unaweza ukaiwekea muda wa ku’expaya. Uzuri ni kwamba hili pia halijaishia hapo pia unaweza ukaifanya barua pepe hiyo kuwa ya usiri wa hali ya juu (Confidential) kwa kuiwezesha kuwa hivyo. Itamladhimu mpokeaji kuingiza neno siri fupi ambalo atatumiwa katika simu yake ili aweze kufungua barua pepe hiyo.

- Nyongeza
Gmail ina mambo mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine inafanya yenyewe kujitofautisha na huduma zingine, kutaka kuyafahamu hauna budi kusoma hapa, na hapa na hapa pia
Tuandikie hapo chini sehemu ya comment hili wewe umelipokeaje? ningependa kusika kutoka kwako je ni njia gani hapo uliwahi kuitumia?
Tembelea TeknoKona kila siku kujipatia habari na maujanja mbalimbali yanayohusu teknolojia na sayansi kwa ujumla. Kumbuka TeknoKona daima tupo nawe katika teknolojia!.