Mnamo tarehe 4/4/2019 Google katika ukurasa wao wa taarifa imesema wameongeza kitu kipya au kwa lugha rahisi tunaweza kusema “Mbwembwe” kwenye Gmail.
Ukiwa kama mtu ambae unafanya wmawasiliano kwa njia ya barua pepe kupitia Gmail utakuwa umeweza kubaini maboresho mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwekwa huko kwa ajili ya kurahisisha vitu lakini kuifanya iwe bora zaidi na hata kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia. SIku kadhaa zilizopita Google wameongeza kitu kizuri kama muendelezo wa kushehrekea miaka kumi na mitano tangu kuanzishwa kwao (Gmail).
Kama wewe ni kati ya wale ambao wanapenda kuandika kichwa cha habari barua pepe baada ya kumaliza kuandika unachotaka kumueleza yule utakayemtumia barua basi utafurahia jinsi Google walivyorahisisha mambo; uwezo wa kutabiri kichwa cha habari kwenye barua pepe (subject) kulingana na kile ambacho mtu amekiandika kwenye uwanja wa kuandika ujumbe kwenye Gmail.
Uwezo huu unategemewa kupatikana kwa kila mtumiaji wa Gmail mnamo Apr, 23 2019. Kipengele hicho kipya kitakuwa mkombozi kwa wengi wetu ambao sio rahisi kupata kichwa cha habari kuhusu ujumbe husika.
Kipengele kipya kwenye Gmail kinachowezesha kutabiri kichwa cha habari.
Teknolojia iliyo nyuma ya pazia inaitwa SMART COMPOSE; kitu ambacho kinafanyika ni kupendekezea maneno ya kuandika kukamilisha sentensi yako kulingana na herufi za mwanzo au maneno kama hayo ulishawahi kuyatumia huko nyuma ulipokuwa unamuandikia mtu ujumbe kupitia barua pepe.
Hii huduma imewezeshwa moja kwa moja na Google lakini unaweza kuizima na kuiwasha kupitia mpangilio (settings>>general>>smart compose) wa akaunti yako iwapo haupendezwi nayo. Je, kipengele hicho kitakusaidia kuweza kuandika ujumbe wako ndani ya Gmail kwa haraka zaidi?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.