Gmail Yatimiza Miaka 15 Huku Ikija Na Maboresho Mapya! #2019

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Gmail ni moja katika ya bidhaa za Google ambazo ni maarufu sana na pia moja kati ya zile zenye watumizi wengi zaidi. Katika masuala ya kutuma na kupokea barua pepe mtandao wa Gmail ni ndio wenye watumiaji wengi.

Logo Ya Gmail

Nembo ya Gmail

Ndio, hali halisi ndio hiyo mtandao wa Gmail uliwekwa hewani kwa mara ya kwanza miaka 15 iliyopita katika sikukuu ya Aprili Mosi. Kwa sababu tarehe hii inajulikana kama siku ya wajinga duniani basi watu wengi walidhani ni kamchezo tuu ambako kanachezwa  na kampuni hiyo.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kuhifadhi na Kutumia Mfumo wa Android kwenye Kompyuta Yako

Ukiachana na Google kuwa kampuni kubwa sana duniani na yenye bidhaa nyingi, kuna bidhaa kwa namna moja au nyingine waliamua kuachana nazo (pengine labda zilikuwa hazileti faida) mf. Google Plus.

Gmail inakuja na maboresho, maboresho hayo ni ikiwemo na uwezo wa kuandaa barua pepe na kuiseti ili imfikie muhusika baadae. kwa mfano unaweza ukaandika barua pepe leo na kuiseti ijitume yenyewe baada ya siku mbili.

INAYOHUSIANA  Datally, app kutoka Google: Njia ya kuokoa utumiaji data wa apps kwenye simu yako

Hili ni jambo zuri sana kwani linarahisisha mambo mengi  hebu fikiria mtu unaweza kandika barua pepe Jumamosi jioni (sio muda wa kazi) na kupanga ijitume katika ofisi fulani Jumatatu saa mbili asubuhi (muda wa kazi).

Pia, katika maboresho hayo kuna kipengele kingine kinajulikana kama ‘Smart Compose‘ kipengele hiki kinasaidia katika uandishi wa barua pepe. kinasaidia kuweza kutabiri neno au kumalizia maneno wakati wa kuandika.

INAYOHUSIANA  Goolge + Yatimiza Miaka 5: Tungalie Maendeleo Yake Kwa Ufupi!

Smart Compose kazi yake nyingine ni kukusoma  jinsi unavyoandika barua pepe ili kujiwezesha kuotea baadhi ya maneno utayokua unataka kuyaandika kabla hujayaandika/hujamaliza yaandika.

Timu nzima ya TeknoKona, kwa ujumla tunasema heri ya siku ya kuzaliwa kwa Gmail.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona. Kumbuka Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.