Facebook imekubali kuwa imeanza rasmi kuonyesha picha zenye mfumo wa GIF. Mfomo huu ni mzuri na watumiaji wengi wa facebook mara kwa mara walionyesha hisia zao kuwa wanauhitaji sana mfumo huu. GIF ni mfumo ambao unaruhusu picha kucheze cheza au kubadilika badilika, mfumo huu kwa haraka haraka unafanana na video lakini sio video.
Mfumo huu umeachiwa kwa facebook ya kwenye kompyuta na hata ile ya kwenye simu (kila mtu atapata!). Wote tujiandae kuona picha zilizo katika ‘Animation’ katika facebook
“Tunaachia mfumo huu wa GIF katika facebook. Na hii ni ili watu waweze ku ‘share’ vitu vya kufurahisha zaidi, na vyenye hisia kwa marafiki zao wakiwa facebook” — Kampuni ilisema
Baada ya kujua hayo kuna lingine la muhimu kulijua naloo ni: Kwa kuongezwa kwa kipengele hiki, watumiaji kwa mfano watakuwa hawana uwezo wa ku ‘upload’ GIF lakini wataweza kuweka link ya hizo GIF. Kuna sehemu nyingi sana (website) ambapo links za GIF zinaweza zikapatikana kwa mfano kama vile Giphy naImgur na facebook wanahakikisha watu kuwa GIF zinaweza zikatokea kukote kama link hiyo itaishia na .gif na isitumie Link iliyofupishwa au iliyobadilishwa.
Watu wanaweza weka GIF hizo katika profile zao na kwa sasa haiwezekani kuweka GIF katika page za biashara kwa mfano page ya TeknoKona. Kwa kuweza kufanya hivi hii inaonyesha kuwa mtumiaji wa facebook hata pata tabu juu ya kuweka GIF hizo itambidi tuu anakili hiyo link na kuiweka kama ilivyo (ku Copy na ku Paste) katika sehemu yake ya kuandika status.
No Comment! Be the first one.