Solar Impulse 2(Si2) ni jina iliyopewa ndege ya kwanza kurushwa na rubani huku ikitumia umeme wa nguvu ya jua, mradi huu ambao pia umepewa jina la solar impulse unafadhiliwa na Andre Borschberg pamoja na Bertrand Piccard ambao pia wanashiriki kama marubani wa ndege hiyo.

Solar Impulse 2(Si2) inapanga kuizunguka dunia kutokea Abu Dhabi kuelekea Oman, India China Japan hadi Marekani ambako inatarajiwa kusimama katika miji mitatu tofauti kabla haijavuka bahari ya atlantiki na kisha kutua ulaya kusini ama Moroko ambako itakamilisha safari yake had Abu Dhabi kituo ilipoanzia safari.

Mbali ya marubani wake wawili ambao watairusha kwa zamu ndege hiyo kuna timu ya watu 60 ambao wanawasaidia marubani hao timu hii ipo Monaco. Si2 inamabawa marefu zaidi ya yale ya ndege aina ya Boeing 747, pia ni nyepesi zaidi (2,300 Kg)ikilinganishwa na Boeing 747 ambayo ina uzito wa kilogramu 440,000.

Safari ya Si2 inategemea hasa uwepo wa jua kwaajiri ya kuchaji betri zake za lithium ambazo ndizo zinazotumika kuiendesha ndege wakati wa usiku. Pia hii ndege huruka na kutua kwa nyakati za usiku, hii ni kwasababu ya wepesi wake maana kwa wakati wa usiku upepo unakua hauna speed kubwa saana. Ingawa hii ni hatua kubwa katika tafiti juu ya usafiri ulio rafiki na mazingira lakini baado tunasafari ndefu mpaka kufikia hatua kwa ndege za kawaida za abiria kutumia umeme wa nguvu za jua.
One Comment