Kivinjari cha Safari ni maarufu sana katika vifaa kutoka Apple, kwa sasa kina watumiaji zaidi ya bilioni moja duniani kote.
Wengine wanasema kuwa namba hiyo ya idadi mbona ilifikiwa mapema tuu lakini ni kwamba kampuni haikutaka kuliweka hilo wazi.
Kingine ambacho kimefanya namba hiyo kuongezeka sana ni kwamba kivinjari hicho ndio kivinjari mama– chaguo-kuu/chaguo-msingi (default browser).
Ukitaka kujua namba yeneywe ambayo wamefikia kwa sasa ni 1,006,232,879 na kukifanya ni kivinjari cha pili ambacho kina watumiaji Zaidi ya bilioni moja.

Ukiachana na kivinjari hicho kuwa cha pili na kupata namba kama hizo lakini bado kipo mbali sana ukilinganiasha na kivinjari ambacho ndio namabari moja.
Google chrome ndio kivinjari namba moja na kina Zaidi ya watumiaji billion tatu. Namba hii tuu inamaanisha kuwa imeviacha mbali sana vivinjari vingine.
Kumbuka kufikia bilioni vipi Safari na Chrome tuu, vingine bado vipo katika mamilioni.
Uzuri wa kivinjari cha Chrome kinapenda sana na kinatumika katika vifaa ambavyo huwa zina vivinjari mama

Mfano kivinjari hiki kinaweza kutumika katika vifaa vya Apple na Windows, Hii haimaanishi kwamba vivinjari vingine havina sifa hiyo—ila ni mapendeleo ya watu tuu.
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Kivinjari >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, niambie unapendelea kutumia kivinjari gani?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.