fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Facebook Mtandao Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Facebook Wameanzisha Scrapbook Kwa Ajili Ya Picha Za Watoto!

Facebook Wameanzisha Scrapbook Kwa Ajili Ya Picha Za Watoto!

Spread the love

150331101603-facebook-scrapbook-babies-780x439

Facebook wameanzisha kipengele kipya Jumanne hii kinachoitwa Scrapbook, Ambayo inawezasha wazazi kutengeneza na kushare albamu (Za Picha)  za watoto wao.

Scrapbook ni tofauti na kwa picha za kawaida katika facebook. Wazazi wana mamlaka ya kutoa vibali nani aone picha hizo  na kivipi watag watoto wao. Wazazi tuu ndio watakua wanaweza kutoa mchango na mtu mwingine hawezi kutoa mchango wake isipokuwa kuona tuu hizo picha kama wazazi wataruhusu

SOMA PIA  CES 2016: LG Kuonesha Kioo (screen) Chao cha Kukunja

Scrapbooks inapatikana katika facebook ya mtandao na hata katika App yake ya kwenye simu. Ili kupata kiengele hiki wazazi inabidi waorodheshe watoto wao kama watoto wao katika sehemu ya wanafamilia katika taarifa za mahusiano (Relationship information).  Wanaomiliki wanyama wafugwao wa mapambo (pet) pia wanaweza tengeneza Album zao lakini inawabidi kuwaorodhesha hayo wanyama.

facebook-scrapbook-1

Facebook pia iliripotiwa kuwa na mpango wa kuwa na kipengele ambacho kitaweweza watoto kwenye Scrapbook kumiliki akaunti hiyo kipindi pale wanapofikia miaka 13 na wataruhusiwa kujiunga facebook wenyewe

SOMA PIA  Messenger Inataka Kuleta Huduma Ya End-To-End Encryption Kama WhatsApp!

Facebook bado hawajajua wataendesha vipi Scrapbook kwa familia zenye watu wengi kama vile watoto wa kambo, watoto wa mjomba n.k kwa sababu kwa sasa ni wazazi wawili tuu ambao wanaweza kutumia Scrapbook

Facebook wamekua bize hivi karibuni kwa kuwa wametoa vipengele vingi sana kama vile kuifanya Messenge kuwa zaidi ya Messenger. Hata kutangaza “Look Back” ambayo inawezesha watumiaji kuona picha ambazo walituma siku husika kwa miaka ya nyuma. Kampuni pia lilifanya mkutano wake wa F8 ambapo waliifanya Fb Messenger kuwa inajitegemea.

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania