fbpx
apps, simu, Teknolojia

Tegemea Kuback Up Chati Za WhatsApp Katika Google Drive!

tegemea-kuback-up-chati-za-whatsapp-katika-google-drive
Sambaza

intaneti-apps-tanzania-simu

Kwa sasa kuback up na kupakua mafaili uliyohifadhi ya whatsApp sio kitu kigumu. Sawa kila mtu anaweza akawa anaweza hili lakini vipi pale unapoibiwa, poteza au hata badilisha simu?

Inakua kazi ngumu, au sio?.Tatizo hili linawakuta mara nyingi watumiajj wa simu za Android.

Unaweza ukabadili simu yako lakini ukapata maudhi kidogo kwa sababu chati zako (za WhatsApp) ulizifanyia back up kwenye memori kadi ambayo umeuza ikiwa katika simu. Sasa unafanyaje?

INAYOHUSIANA  Samsung: Samsung Galaxy S10 ni familia ya simu nne! Fahamu vipya kutoka Samsung

Fununu zinasema kuwa WhatsApp wanaweza wakaanzisha mfumo mpya wa kufanya back up na hiyo itakua inafanyika na Google Drive. Hii itarahisisha kila kitu kwa sababu mtumiaji wa whatsapp anaweza fanya back up mda wowote na kwa urahisi tuu.

Watumiaji hawatafanya kazi kubwa kwa mikono yao bali kila kitu kitakua kikifanyika kirahisi tuu. Sio lazima mpaka waweke memori kadi zao. Hata hivyo kitu ukikihifadhi katika mtandao ndio kina nafasi kubwa ya kudumu kuliko kikiwa katika simu.

INAYOHUSIANA  Asilimia 40 Ya Watuamiaji Wa iPhone Watahama Kama Watapewa Bure Simu Ya Android! #Tafiti #iOsVsAndroid

MUHIMU: Kwa sasa Back Up iliyochukuliwa katika simu ya Android itatumika tuu kwenye simu za Android, Pia itakua hivyo hivyo kwa simu za  iOS, Windows na Blackberry. 

Mabadiliko haya yatakua mazuri na yatapokewa sana na watumiaji wa Android, Windows na Blackberry. Watumiaji wa iOS kwa sasa wanafanya Back Up za chati zao za whatsApp katika iCloud. Kwa hiyo katika iPhone itakua ni chaguo la ziada na sio kitu kipya.

INAYOHUSIANA  Dola Bilioni 24! Snapchat yazidi kujidhatiti katika soko la hisa

Kama teknolojia hii ya ku backup WhatsApp  katika Google Drive ikiwezeshwa, itakua ya msaada mkubwa kwa watumiaji wa sim za Android,Windows na Blackberry.  Ngoja Tuone jinsi itakavyo kuwa pale teknolojia hii itakapoanza tumika.

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*