Miaka 40 iliyopita tarehe 4 mwezi wa nne mwaka 1975 Bill Gates na Paul Allen walianzisha kampuni ya Microsoft. Kwa kuanzia walikuwa wanatengeneza programu ambayo kwa wakati hiyo ilikuwa inafahamika kuwa katika familia ya BASIC Interpreters.
Programu mbalimbali za matumizi madogo, wakati huo katika akili zao hawakufikilia kwamba kampuni wanayoanzisha ingekuwa moja kati ya kampuni kubwa duniani katika eneo la programu endeshaji (OS) pamoja na programu za kazi mbalimbali mfano ‘MS OFFICE’.
Katika miaka 40 ya kampuni hiyo imekua na kusambaa kutoka utengenezaji wa programu tuu hadi kuingia katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki kama vile kifaa cha kuchezea magemu cha XBox na pia kwenye tableti kwa kuja na Surface..na bila kusahau uamuzi wao wa kununua kampuni ya Nokia na hivyo kuingia rasmi katika utengenezaji wa simu.Kwa sasa ni vigumu sana katika kazi za kila siku mtu asitumie kitu kutoka Microsoft. Kama usipotumia programu uendeshaji yao ya Windows basi unaweza ukajikuta unatumia programu za kiuandishi yaani Microsoft Office – Word, Excel, Powerpoint, Outlook n.k
“Tumefanikisha mengi pamoja katika kipindi cha miaka yetu 40 na kuwezeshwa biashara na watu mbalimbali kufanikisha mambo yao. Lakini jambo la msingi kwa sasa ni nini tunafanya baada ya hapa”, Bill Gates.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo kwa sasa Bwana Satya Nadella amepewa sifa sana za kuweza kufanya mabadiliko katika kampuni hiyo yanaoonesha kuleta mafanikio sasa na mbeleni. Chini ya uongozi wake kampuni ya Microsoft imefanikiwa kuweka kipaumbele kwenye eneo la teknolijia ya Cloud, simu na tableti pia, hii ni pamoja na kuleta apps zake za Office kwa watumiaji wa simu za iOS na Android.
Mambo mengi mazuri yanakuja hao baadae mwaka huu, hii ni pamoja na toleo la Windows 10 ambalo litaweza kufanya kazi kwenye kompyuta, tableti na simu. Na hivyo kuraisisha kwa sana kazi ya utengenezaji apps kwa ajili ya Windows 10. Pia toleo la Office 2016 kwa ajili ya Windwos na Mac litatolewa pia.
Hadi sasa mambo yanaonekana yanaenda vizuri sana kwa kampuni hii, TeknoKona tunawatakia miaka 40 mingine ya ubunifu na mafanikio zaidi.
Soma Pia;
Mambo 16 Ya Ukweli na ya Kuvutia Kuhusu Bill Gates!
Makala yote kuhusu toleo lijalo la Windows 10!
No Comment! Be the first one.