fbpx

Njia Mbalimbali za Kushusha Video kutoka YouTube!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

download youtube videosIwe kupitia simu yako au kwenye kompyuta wengi tunapenda kuwa na baadhi ya video tunazozipenda ili tuweze kuzitazama tena na tena. Zifuatazo ni njia mbalimbali za kukuwezesha kushusha ( kimombo-Download) video mbalimbali kutoka Youtube na ata mitandao mingine. Usisahu kusambaza makala kwa wengine pia.

Kwenye MTANDAO.

 

ClipConverter (Mtandao)

ClipCoverter ni mtandao unaopatikana kwa anuani ya http://www.clipconverter.cc/ , kupitia mtandao huu unaweza kushusha video mbalimbali kutoka mitandao mbalimbali si Youtube pekee. Unachotakiwa kufanya ni kwenda na kukopi anuani (pale kwenye www.yo……) ya video unayoitaka.Ukishaikopi unarudi kwenye mtandao huu wa ClipConverter na kuiweka kwenye ‘Media Url Download’ na kushusha na kumbuka unaweza ukachagua aina ya mfumo (format) unaitaji. Hii inaweza kuwa MP3, MP4 3GP na zingine nyingi.
Muonekano wa sehemu ya kushusha-ClipConverter
INAYOHUSIANA  Tigo na 4G: Smile Yapata Ushindani! Je tupo tayari kwa 4G?

 KeepVid (Mtandao)

 KeepVid inapatikana kwa anuani ya http://keepvid.com/ nayo kama ClipConverter unaweza shusha video kupitia kuweka anuani ya video hiyo kwenye mtandao huo. Haina tofauti sana na ClipConverter tukitoa chaguo la mifumo mbalimbali ambalo halipo kwenye KeepVid.

 Mitandao mwingine ni SaveVid, nao mfumo wake unafanana na hizo za juu.

Video DownloadHelper

Njia nyingine rahisi sana na maarufu ni kwa watumiaji wa Firefox, hii ni kwa kutumia ‘Extension’ maarufu ya Video DownloadHelper. Video DownloadHelper ni kitu kinachoingia kwenya Firefox. Kukishusha na kupakua (install) kwenye Firefox yako bofya hapa. Hii inaurahisi zaidi kwani haitahusisha kukopi anuani zozote, yenyewe itakuwa inatambua kama ukurasa wa mtandao unaotembelea unavideo au faili la sauti linaloweza kushushwa. Na ikitambulika hivyo kialama chake kwenye Firefox kitaanza kuzunguka. Ukikibofya tu itakupa chaguo la kushusha video hiyo na unauwezo wa kuchagua mfumo unaoutaka. 

Muonekano wa Video DownloadHelper Kama Hakuna cha Kushusha

Muonekano wa Rangi unabadilika na Ukibofya kwenye Kialama unapata chaguo mbalimbali za Mifumo(format)

download youtube videos via desktopKWA KUTUMIA PROGRAMU ZA KOMPYUTA.

Kuna programu nyingi sana za kutumia ila nitakupa moja ambayo ni maarufu inapokuja kwenye sifa ya utendaji kazi na ni ya bure.

Freemake [Windows]

Freemake ni programu yenye muonekano mzuri na pia inakupa uchaguzi mzuri wa kile unachotaka kushusha. Unaweza badili mfumo na ata kiwango cha ubora wa video ili kupunguza ukubwa wa faili. Na zaidi ya yote ni programu ya bure kabisa. Kushusha na kuingiza kwenye kompyuta yako bofya hapa

 

INAYOHUSIANA  HarmonyOS: Programu endeshaji ya Huawei yatambulishwa rasmi. #HDC

Muonekano wa Freemake

download youtube videos via mobile devices KUSHUSHA KUTUMIA SIMU YAKO

 

TubeBox(iOS)

Hii ni kwa wanaotumia iPhones au iPads (ios). Kupitia TubeBox utaweza kutafuta na kuangaliza video mbalimbali kutoka Youtube na pia utakuwa na uwezo wa kuzishusha na kuweza kuzitazama tena hata bila huduma ya intaneti. Kushusha bofya hapa.

TubeMate(Android)

Hii ni app nzuri inayokuwezesha kutafuta na kushusha video mbalimbali kutoka Youtube. Na inafanya kazi kwenye simu nyingi za Android, kuishusha bofya hapa.

WonTube (Android)

WonTube ni njia nyingine kwa watumiaji wa simu au tableti za Android. WonTube inakuwezesha kutembelea mtandao wa YouTube ndani yake na utakapoitaka video yeyote kunasehemu ya kubofya ‘Download’ na video hiyo itashushwa na kuhifadhiwa kwenye simu yako. Kuishusha kwenye simu yako bofya hapa.

 

INAYOHUSIANA  YouTube inalipa! Mtoto, Boram anunua jengo la ghorofa 5 la thamani ya dola milioni 8

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

5 Comments

Leave A Reply