fbpx
Apple, Teknolojia

Apple: Hivi Karibuni Utaweza Kuchaji iPhone na MacBooks Mara 1 Kwa Wiki

apple-hivi-karibuni-utaweza-kuchaji-iphone-na-macbooks-mara-1-kwa-wiki
Sambaza

Muda wa vifaa vingi vinavyotumia mfumo wa betri za kuchaji huwa mrefu sana kama vifaa hivyo vitakuwa havitumiwi tumiwi sana na watumiaji wake. Kama Kompyuta pakato au simu janja, huweza kudumu endapo tu mtumiaji atajibana kutomaliza chaji ya kifaa chake, kama kuzima data, kupunguza mwanga n.k.

APPLE KUANZA KUTUMIA MFUMO MPYA WA BETRI UTAKAOENDESHA MACBOOK NA IPHONE KWA ZAIDI YA WIKI BILA KUCHAJI.

Kwa kompyuta pakato, muda wa wastani wa kompyuta hizi kukaa na chaji ya betri ni masaa manne hadi sita. Baadhi ya kompyuta za Apple, mfano MacBook Air, hufikisha hadi masaa 11. Huu ni muda mrefu zaidi ukilinganisha na kompyuta za kawaida. Kwa watumiaji wa simu janja, ni kawaida kila baada ya siku kuisha, kuchomeka simu katika umeme ili kifaa chako kiingize chaji upya.

INAYOHUSIANA  Samsung: Jinsi itakavyokuwa simu ya mkunjo
Mfumo wa sasa wa betri ktk MacBook 12'
Mfumo wa sasa wa betri ktk MacBook 12′

Sasa, hayo yote yatabadilika. Mfumo mpya wa kuandaa betri kutoka Apple utafungua kurasa mpya kwa watumiaji wa vifaa vinavyotumia betri za kuchaji. Jana, washirika wa kampuni ya Apple kampuni ya U.S Patent and Trademark walichapisha mfumo unaolingana na ule wa kampuni ya Cupertino kuonyesha mfumo mpya wa Seli za betri ambao utawezesha kompyuta za MacBook kufanya kazi bila kuchomekwa kwenye umeme kwa muda wa “masiku hadi zaidi ya wiki” Maombi ya leseni ya utengenezaji wa betri hizo yalichapishwa jana huku yakiweka wazi mfumo huo utatumika kwenye kompyuta za MacBook, japo “kompyuta za kawaida” huenda zikahusika.

INAYOHUSIANA  iPhone 6s Yaleta Wateja Wengi Kwa Apple Kuliko iPhone 7! #Ripoti
Mchoro uliochapishwa kuonyesha Mfumo mpya wa Seli zinazotumia mafuta Maalum
Mchoro uliochapishwa kuonyesha Mfumo mpya wa Seli zinazotumia mafuta Maalum

Kinachovutia zaidi ni kwamba, mfumo huu ulishawahi kupendekezwa na kampuni moja ya Uingereza inayohusika na mambo ya nguvu za umeme, na kuzua tetesi kua Betri hizo mpya huenda zikatumika kwenye simu za iPhone 6.

Uvumi umezuka upya na mitandao mbalimbali maarufu imeripoti kuwa huenda mfumo huu ukazinduliwa na simu mpya za iPhone 7 au toleo jipya zaidi la kompyuta za MacBook Air.
Japo si kwa mfumo huu mpya, Apple tayari wamebadili kabisa mfumo wa betri katika toleo jipya la sasa la MacBook Air, katika video waliyoichapisha katika mtandao wao.

INAYOHUSIANA  Apps Zilizoongoza Kushushwa App Store 2014!

Tofauti ya mfumo huu mpya wa betri na ule wa zamani ni katika mfumo wa kuchaji, ambapo Seli mpya za betri zitatumia cartridges zenye mafuta maalumu ambazo zitahitaji kubadilishwa kila baada ya muda fulani. Apple wanaonekana kuupa kipaumbele mfumo huu kwa matumizi ya vifaa vyake vipya.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

iMe

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*