Sony wamezindua toleo jipya la mtiririko wa simu za Xpreria itakayojulikana kama Sony Xperia Z5 katika maonesho ya kimataifa ya kiteknolojia yaliyofanyika Berlin, Ujerumani.
Simu hiyo itakayopatikana katika matoleo matatu kila moja ikiwa na kamera yenye uwezo wa Megapixeli 23 inayoongezewa nguvu na sense thabiti ya Sony, imeongezewa uwezo wa kupiga picha kwa kasi, pamoja na uwezo wa kupiga picha katika mazingira yenye mwanga hafifu.

Simu kubwa zaidi katika matoleo ya Sony Xperia Z5, itajulikana kama Xperia Z5 Premium, na itakuwa na ukubwa wa nchi 5.5. Inakuja na kioo cha ‘resolution’ ya pixels 3,840 x 2,160, hichi ni kiwango kikubwa zaidi cha pixels katika simu janja kuliko simu nyingine nyingi. Hii inakipa kioo chake wastani wa pixel 806 kwa kila inchi wakati kioo cha simu ya iPhone 6 kina wastani wa pixels 326 kwa kila inchi, hii ni tofauti kubwa sana.
Mwanzo, simu za Sony zilikua na uwezo wa kurekodi video zenye pixeli 4K, lakini hazikuwa na kioo chenye uwezo wa kucheza video zenye ubora huo wa pixeli 4k.
Xperia Z5 sasa zinakuja na sensor maalum za kurekodi alama za vidole, kama zile za simu za iPhone 5S na iPhone 6.
Itakuwa na processor inayojulikana kama Qualcomm Snapdragon 810 yenye Octa-core CPU pamoja na uwezo wa intaneti wa 4G. Itakuja na toleo la Android la 5.1.1. Imebeba RAM ya GB 3, pamoja na diski uhifadhi (storage) wa GB 32.
Sony wanasema, upekee wa simu hii ni pamoja na Betri yake ya ndani yenye ukubwa wa 3430 mAh, itakayokuwa na uwezo wa kudumu kwa karibia siku mbili mfululizo.
Simu hii yenye ubora wa hali ya juu kabisa itauzika kwa dola 955 za Kimarekani, hii ni takribani Tsh Milioni 2 za Kitanzania.
Sifa kubwa kwa ufupi;
- Kioo cha ubora wa hali ya juu (4K display)
- ‘Fingerprint sensor’
- Kamera ya ubora wa juu
- Ubunifu wa kiwango cha juu
Ubaya;
- Bei ghari, kutoa milioni mbili kwa ajili ya simu janja si jambo la kawaida. Unatakiwa uwe nazo kweli kweli
- Kiwango cha betri kipo juu ila kutokana na uwezo mkubwa wa simu hiyo chaji inaweza isikae muda mrefu sana
One Comment