Makampuni kadha wa kadha isipokuwa Apple wamejitahidi kuhakikisha bidhaa zao zinapata masasisho (kuhamia) kwenye Android 9 ili kuweza kupata kuona kile ambacho kimeboreshwa.
NOkia wameweka wazi ratiba ya simu zao ambazo mpaka sasa zinafika matoleo kumi na tano kwa idadi; 5 kati ya hizozikiwa tayari zimesharuhusiwa kuweza kupakua programu endeshi toleo la kenda na matoleo mawili mengine mpango wa kuruhusu kuweza kushisha ukiwa unaendelea.
Tayari Nokia 5.1 Plus, 6.1, 6.1 Plus, 7 na 7.1 Plus zimepewa kibali cha kupokea/kuweza kuhamia Android Pie. Huku kwa Nokia 8 na 8 Sirocco zikiwa kwenye mchakato wa kuweza kuruhusiwa kupokea masasisho hayo.
Orodha na lini simu za Nokoa zitapokea masasisho ya Android 9
Simu
Ruhusa ya kuweza kupakua Android 9
Nokia 3.1 Plus
Januari 2019
Nokia 5
Januari 2019
Nokia 2.1
Kwenye robo ya kwanza ya mwaka 2019
Nokia 3.1
Kwenye robo ya kwanza ya mwaka 2019
Nokia 5.1
Kwenye robo ya kwanza ya mwaka 2019
Nokia 6
Kwenye robo ya kwanza ya mwaka 2019
Nokia 1
Mwanzoni mwa robo ya pili ya mwaka 2019
Nokia 3
Mwanzoni mwa robo ya pili ya mwaka 2019
Uwezo wa kupokea masasisho ya Android 9: Mpaka kufikiakufikia mwezi Juni 2019 simu janja nyingi za Nokia zitakuwa zimesharuhusiwa kuweza kupakua Android Pie.
Kama unatumia Nokia 2 basi itakubidi usubiri haijulikani mpaka lini ili kuweza kushusha Android 9 kwani haipo kwenye orodha ya simu za Nokia ambazo zitaweza kushusha toleo hilo la programu endeshi.
Vipi Nokia unayotumia ipo kwenye mpango au tayari umeshahamia kwenye Android kenda?
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|