fbpx
HaloPesa, Halotel, Mitandao ya Simu, simu, Tanzania

Fahamu kuhusu Ninogeshe na HaloPesa

halotel-na-ninogeshe-na-halopesa
Sambaza

Kampuni ya Halotel imetangaza kuondoa gharama za kutuma fedha huku ikiwazawadia muda wa maongezi wateja watakaoweka fedha kwenye akaunti zao.

Halotel inayokuwa kwa kasi imezindua kampeni mpya inayofahamika kama ‘Ninogeshe na Halopesa’ inayowapa pia fursa wateja wa kampuni hiyo kutuma pesa bure ndani ya mtandao (Halotel-Halotel) muda wowote.

Lengo ni kuhakikisha wateja wanakuwa na wigo mpana wa kufurahia na kunufaika zaidi na huduma za mtandao huo bila kuwa na wasiwasi wa makato kila wanapotuma fedha mahali popote, wakati wowote.

Ninogeshe na HaloPesa
Kampeni hii ni maalum kwa wateja wote wa Halotel waliopo mjini na vijijini wanaokupitia HaloPesa.

Licha ya kuondoa gharama za kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda Halopesa, pia wateja watapata muda wa maongezi wa bure kila wanapoweka fedha kwenye akaunti zao:

INAYOHUSIANA  Maana ya "TTY Mode" kwenye rununu

Mteja atakapoweka kuanzia Tsh. 1,000 kwenye akaunti yake  kupitia wakala wa HaloPesa atazawadiwa muda wa maongezi huku akiendelea kunufaika kwa namna mbalimbali kila anapotumia huduma hiyo.

Ninogeshe na HaloPesa
Vilevile, Halotel imepunguza gharama za kutuma fedha kwenda mitandao mingine.

Huduma ya HaloPesa ina miaka miwili sasa tangu ilipoingia sokoni na kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni mwendelezo wa adhma ya kuboresha huduma za fedha kwa njia ya mtandao kwa wananchi wenye vipato tofauti.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.