Nilipokea ujumbe mfupi wa maneno leo asubuhi mida ya saa 5 kutoka tigo ‘Kutokana na kukatika kwa mkonga baharini mtandao wa tiGO intaneti hautopatikana. Mafundi wetu wanafanya jitihada kurekebisha tatizo. Tunaomba radhi kwa usumbufu’.
Hadi muda huu, takribani saa tano usiku bado kwangu na kwa wengine niliowasiliana nao huduma ya intaneti bado haipatikani.
Matatizo haya yamezidi kujitokeza kwa sana, ushauri pekee kwa tiGO kama ni suala la mkonga wa intaneti basi kuna ulazima wa kutotegemea sehemu moja tuu ya uunganishi wa huduma hii muhimu.
Imekua siku mbaya sana kwa watu wote wanaotegemea huduma za intaneti kutoka tiGO, ni muhimu kuepusha janga kama hili kwa kuhakikisha kuna vyanzo vingine pale ambapo chanzo kikuu kinakuwa na matatizo.
No Comment! Be the first one.