Mitandao yetu ya simu huwa inatuma mipangilio(settings) ya huduma za intaneti lakini mara nyingi imegundulika hawajafanya mabadiliko ya mipangilio hiyo ili iendane na simu za kisasa na matokeo yake mipangilio hiyo inashindwa kufanya kazi. Hii inatokea kwa simu nyingi hasa za mfumo wa Android.
Hivyo Teknokona tumeona ni vizuri upate kuondoa usumbufu wa kuhangaika kuwezesha huduma hii muhimu kwenye simu yako. Fuata maelekezo haya yaliyoambatana na picha ili uwezeshe huduma hii kwenye simu yako.
Kitu kidogo tunawezesha ni kile kinachojulikana kama ‘APN: Access Point Name’, kwa simu za android APN ikiwa sahihi tuu basi mara moja simu yako itaweza pata huduma ya intaneti.
1. Simu yako ikiwa imewashwa, nenda ukurasa wa menyu.
2. Nenda ukabofye kwenye ‘Settings’
3. Bofya sehemu ya juu, kwenye ‘Wireless and Networks’
4. Kisha kwenye Wireless and Network’ shuka chini kabisa utaona ‘Mobile Networks’, bofya hapo.
5. Hakikisha kwenye ‘Use Packet Data’ pametikiwa, kisha bofya kwenye ‘Access Point Names’
6. Ukifika hapo bofya sehemu ya kukuonesha chaguzi/’options’, utaona kwa chini utapewa chaguzi mbili, bofya kwenye ‘New APN’
7. Kisha bofya kwenye ‘Name’ andika jina la mtandao wako, hii nimeona haiathiri uwezo wa kuunganisha kwenye intaneti. Kisha bofya ‘Ok’.
8. Kisha bofya kwenye APN, hapa ndipo muhimu, andika ‘internet’ (kwa Zantel andika znet) hakikisha ni herufi ndogo. Kisha bofya ‘Ok’
9. Hakikisha mambo yapo sawa kama kwenye hii picha, kisha bofya kurudi nyuma, utaona mpangilio wako upo sawa. Hakikisha umechaguliwa.
Na hakika utaona alama ya ‘E’ au ‘3G’ kwenye ‘notification center’ yako
NB: Mipangilio hii inafanya kazi kwenye mitandao ya Vodacom, Tigo na Airtel, kwa Zantel kwenye APN andika ‘znet’
ktk s3 shv e210L haileti intaneti