Watu wengi wanajiunga Twitter kwa sasa Tanzania, na wengi wangependa kuunganisha akaunti zao ili kurahisisha kutuma hali zao (‘status’ zao).
Makala hii itakuonyesha jinsi ya kuungannisha akaunti yako ya Twitter na Facebook ili Tweets zako moja kwa moja baada ya wewe kuziposti zitokee pia kwenye akaunti yako Facebook.
1: Ingia kwenye akaunti yako Twitter
2: Nenda kwenye ‘Settings’
3: Shuka eneo la chini na bofya sehemu iliyoandikwa ‘Sign in to Facebook and connect your accounts’
4: Baada ya hapo chagua nani waone tweets zako kwenye ukurasa wa Facebook, je ni marafiki au mtu yeyote. Kawaida huwa zipo zionekane kwa kila mtu.
5: Bofya ‘Log in with Facebook’ kisha ingiza taarifa zako za Facebook
6: Bofya ‘Allow’
7: Sasa Tweets zako zitakuwa zinatumwa pia kwenye ukurasa wako wa Facebook kama ‘status’, ila tweets za majibu kwa watu wengine twitter hazitakuwa zinatumwa Facebook.
Usisite ku’share’ kwa wengine makala hii.
No Comment! Be the first one.