Makampuni ya Samsung na Apple wamekuwa na kesi nyingi zaidi za kushitakiana huku kila mmoja akiwa anadai suala flani mwenzake amemuiga hasa kwenye masuala ya mitindo, staili na teknolojia zingine wanazotumia kwenye simu na tableti.
Kwenye tangazo hilo, ambalo unaweza liangalia hapo chini, unaonesha watu waliokuwa wakiudhuria harusi wakianzisha ugomvi ambao ukahusisha watu wote baadae. Lakini ugomvi huo utakuwa mkubwa ukihusisha pande nzima ya watuamiaji wa bidhaa za Apple na wale wa za Samsung.
Kisha tangazo linaonesha watumiaji wa Nokia Lumia 920 wakiwa wanawashangaa na kujiuliza kama watu hawa wangejua kuna Nokia Lumia 920 wangeendelea kupigana hivi, mmoja akajibu
“Nadhani wanapendelea kupigana”. Tangazo hili limepata umaarufu sana, nawe unaweza liangalia hapa chini.
No Comment! Be the first one.