Ushindani katika kupunguza gharama za huduma ya maongezi ya simu Tanzania inazidi kupamba moto na wateja kuzidi kunafaika. Kampuni ya Vodacom hii leo imebadili mfumo wa huduma ya Cheka Nao.
Kabla huduma hiyo ilikatika itakapofika saa sita usiku bila kujali mteja alijiunga saa ngapi siku hiyo. Kwa sasa huduma hiyo itakuwa inakaa kwa muda wa masaa 24 tokea mteja ajiunge. Kupitia ukurasa wao wa Facebook na Twitter wametoa taarifa ya mabadiliko hayo.
SASA CHEKA NAO KWA MASAA 24! Kuanzia Tsh 350 ongea DAKIKA 10 mitandao yote nchini bila ya mipaka MASAA 24 baada ya kujisajili. Piga *149*01#
— Vodacom Tanzania (@VodacomTanzania) May 3, 2013
No Comment! Be the first one.