fbpx
Android, Android Pie, Samsung, simu, Teknolojia

Android 9 yaboreshwa kwa mara ya pili kwenye Galaxy Note 8

android-9-yaboreshwa-kwa-mara-ya-pili-kwenye-galaxy-note-8
Sambaza

Ukiwa kama mtu ambae hupendi kuifanya simu janja yako ikose vile vitu ambavyo wahusika wanaviboresha basi utakuwa ni mtu ambae unapakuwa unaangalia iwapo kuna masasisho yoyote yameletwa kwenye programu endeshi husika.

Kwa wale ambao wanatumia Samsung Galaxy Note 8 na pia Android 9 ikiwa ndio programu endeshi iliyopo kwenye rununu husika basi watakuwa wamekupana na matatizo kadhaa kiasi ambacho Samsung imewabidi kuleta maboresho ambayo yamalenga kuondoa kero hizo.

Masasisho hayo ni ya pili lakini sio rasmi (yapo kwenye hatua ya majaribio-BETA) na yamelenga kutatua mambo yafuatayo:-

kamera kujifunga pale mtu anapochukua picha jongefu katika mwendo wa polepole, kuganda/kutoonekana vizuri kwa kipengele cha “viewfinder“, miziki/kitu chochote kinachoshushwa kutoka mtandaoni kutoonekana kwenye memori ya ziada pale inapotunzwa huko.

Galaxy Note 8
Sasisho la Android 9 kwenye Samsung Galaxy Note 8-linachukua MB 705 kuweza kulishusha.

Sasisho hilo pia linatazamiwa kuruhusiwa kwenye Samsung Galaxy S8 na S8+ katika siku za usoni lakini kumbuka kuwa na angalau MB 800 ili kuweza kupakua sasisho hilo au utumie WI-FI bila kusahau chaji ya kutosha (asilimia 50+).

Vyanzo: SamMobile, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Walemavu wa kusikia na matumizi ya simu Tanzania
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|