WhatsApp licha ya ukubwa ambayo mpaka sasa inayo, bado haijawahi kupumzika katika kuhakikisha kuwa inakuja na mambo mapya na maboresho mengi katika huduma yake.
Mitandao mingi inatoa huduma za simu za makundi, na kuna mitandao mingine ni mahususi kabisa katika kupiga simu za video au kuendesha mikutano kwa njia hiyo mfano mzuri ZOOM. WhatsApp na yenye haijataka kubakia nyuma kabisa.

Kwa sasa katika huduma hiyo ya kwenye kompyuta simu 8 za video zinaweza fanyika huku zile ambazo sio za video –za sauti– zinaweza kubeba watu mpaka 32.
Kumbuka Meta ulinziasha App kabisa ya WhatsApp katika Windows na App hii inakubali katika Windows 10 na kuendelea tuu.
Na tangia ianzishwe – katika windows – kuna mabadiliko makubwa kwa maana ya maboresho na jambo hili limefanya mtandao huo uwe na ufanisi wa hali ya juu.

Sio mara ya kwanza kwa huduma ya WhatsApp kupatikana katika kompyuta ila kulikua na namna ambavyo inapatikana eidha kwa kutumia WhatsApp Web au kwa namna nyingine ukiachana na App kabisa.
Jambo la kuwa na uwezo wa kuwezesha watu nane katika simu moja ya video ni jambo kubwa sana na hii inapendeza hata kwa wale ambao watatumia huduma hii katika kuendesha mikutano yao.
Hebu fikiria hapo zaman watu walikua wanaweza kabisa kupanga mipango ndani ya mtandao wa WhatsAppp (labda muda wa kikao, ajenda ya kikao n.k) na mwisho wa siku kikao hiko kinaenda kufanyika katika mtandao mwingine kama vile ZOOM.
Kama unataka kushusha App ya WhatsApp katika kompyuta yako ya windows 10 au zaidi unaweza kuingia >> HAPA << hapa sasa na ushushe App hiyo
Kwa watumiaji wa Mac kampuni imesema kuwa inajitahidi katika kuhakikisha inawaletea App katika vifaa hivyo, hivyo basi hawana budi kusubiri japo hatua za mwanzo tayari ..soma zaidi >>HAPA<<.
Soma >>HAPA<< pia, tuliandika kuhusiana na App ya WhatsApp Kwa Tabiti za Android.
Ningependa kusikia kutokea kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kwa hatua hizi ambazo WhatsApp wanazichukua unadhani wanaweza kuzipiku App nyingine nyingi za maswala ya video
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.