Ukaichana na mtandao wa WhatsApp kuwa maarufu sana kama njia ya haraka ya mawasiliano, bado mtandao unajikita katika kuhakikisha kuwa inawapa wateja wake kile wanachokitaka.
Ukaichana na mtandao wa WhatsApp kuombwa kipengele hiki kwa muda sasa, wao wameamua kukiachia na kinachofanyika hapa ni kwmaba utakua na uwezo wa kutumia namba moja –unayoitumia WhatsApp– katika vifaa viwili.
Kwa sasa hili limewezekana lakini inawezekana ikawa sio kama unavyofikiri, hapa kidogo kuna jambo ambalo pengine linaweza lisikufurahishe.
Kwa sasa jambo hili linawezekana kama una Tabiti (tablet) ya Android na simu janja –ya android– unaweza ukaunganisha vifaa hvyo na vikawa vinapoakea meseji na kujibu kwa pamoja tuu.
Hapa hakuna kilichobadilika sana hii ni kama tuu ile ya simu na kompyuta (ya mtandao) inavyofanya kazi kwamba vifaa vyote viwili vinaweza vikafanya kazi kwa pamoja tuu.
Kitakuachokua kinafanyika ni kile kile utaweza kutumia huduma hii kwa kutumia QR code ambayo itakua ikionekana katika WhatsApp ya tabiti ya Android.
Kwa sasa jambo hili linawezekana na lipo katika mfumo wa Beta –ambao ni mfumo wa majaribio – lakini ni wazi kuwa baadae mfumo mzima utaanza kupatikana kwa watu wote.
Vile vile unaweza ukajitoa kutumia mtandao huu katika tabiti hiyo mara tuu ukiamua kufanya hivyo ili kubakia na kutumia simu yako ya kawaida tuu.
Kwa mwaka huu pengine katika mitandao ya kijamii WhatsApp ndio inaweza ikawa imeweka rekodi ya kuwa na masasisho (update) mengi sana.
Ukiachana na hayo ote ni wazi kuwa bado mtandao wa WhatsApp unapambana sana katika kuhakikisha kuwa unazidi kubakia katika nafasi za juu kabisa huku ukizidi kukonga nyoyo za watumiaji wake.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani unaweza ukawa unatumia WhatsApp kwenye Tabiti na kwenye simu janja?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.