Mtandao wa Twitter umeleta kipengele kinachoitwa “Happening now” ambacho ni mahususi kwa ajili ya kukusanya Tweets ambazo zinaongelea tukio fulani.
Hii inachukuliwa na wachambuzi wa mambo kwamba ni moja ya hatua za mtandao huu kujaribu kujikwamua katika matatizo yake ya kiuchumi.
Feel the roar of the crowd, no matter where you are.
We’re rolling out a new way to see what’s happening now, starting with sports in ????????! Available on Android and iOS starting today. https://t.co/lmBFCK4DG0 pic.twitter.com/cv4wL8hCxA
— Twitter (@Twitter) October 10, 2017
Kipengele cha Happening now ni mahusus kwa ajilii kukusanya tweets ambazo zinaongelea tukio moja (mfano mechi ya mpira wa kikapu/mkutano wa siasa au uzinduzi wa filamu). Tofauti na tulivyozoea kipengele hiki hakitatumia alama ya reli (Hashtag) kama kiungo bali maudhui ya tweet ndiyo yatakayotumika kukusanya tweets.
Twitter inajitahidi kuteka soko na kuwa ndio chombo ambacho matukio kama mechi za mpira, uzinduzi wa filamu, mikutano ya siasa na matukio mengine makubwa yanajadiliwa. Hii itausaidia mtandao huu kuweza kuvutia wawekezaji wengi katika sekta ya matangazo hivyo kuongeza mapato ambayo yamekuwa yakishuka.

Happening now inataka kufanana na Twitter moments ambayo nayo inakuletea mkusanyiko wa tweets mbalimbali kuhusu jambo fulani. Huduma hizi mbili zinatofautiana katika namna mkusanyiko wa tweets unavyopatikana. Wakati kwenye kipengele cha Twitter moments kila mtu anaweza kutengeneza kwa kuzikusanya tweet mbalimbali na Happening now ipo upande wa Twitter wenyewe na ndio wataamua tweets zipi zionekane-watumiaji hawatakuwa na usemi juu ya hili.
