fbpx

Vitu vinavyofanyika kwenye intaneti ndani ya dakika moja #2019

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kila sekunde inayopita basi kuna kitu kinafanyika kupitia intaneti ambapo mpaka kfikia mwaka jana mwishoni imefahamika kuna watumiaji zaidi ya bilioni nne kutoka bil. tatu mwaka 2017 hivyo ambayo idadi yake haipungui bali inaongezeka mwaka hadi mwaka.

Ukuaji wa teknolojia unafanya intaneti kuwezesha vitu vingi ambavyo vinafanyika kila siku ambayo inapita. Hivi leo matumizi ya mtandao ya kijamii, mawasiliano kwa njia mbalimbali, kutafuta vitu mtandaoni, n.k sio vitu vya kushangaza kiabisa bali ni vitu ambavyo vinafanyika kila sekunde na kw wengine imekuwa ni lazima watumie moja ya vitu hivyo ili waweze kufanikisha mambo yao.

INAYOHUSIANA  LAUNDROID: Panasonic Waja na Roboti kwa Ajili ya Kufua, Kukunja na Kupanga Nguo

Ulishawahi kujiuliza “Ni vitu gani ambayo vinafanyika ndani ya dakika moja kupitia intaneti?”. Kwa mujibu wa habari picha kuhusu vitu ambavyo vinafanyika kwenye intaneti ndani ya sekunde sitini (60) imefahamika na unaweza kuotea ni kitu gani kinaongoza kutumiwa zaidi ndani hiyo dakika moja?

kwenye intaneti

WhatsApp ndio imeongoza kwa mwaka 2019 kwa jumbe nyingi kutumwa ndani ya dakika moja.

Tulinganishe mwaka 2018 na 2019

Kwa kulinganisha miaka miwili (2018/19) takwimu zinaonyesha watumiaji wanazidi kuongzeka kwa kiasi kikubwa tuu huku Instagram na Netflix watumiaji wake wakiongezeka kwa kasi lakini bado WhatsApp ikiwa ni kinara na ikifuatiwa jumbe za kawaida.

kwenye intaneti

Yaliyoweza kufanyika kwenye intaneti ndani ya dakika moja kwa mwaka 2018 na 2019.

Hayo ndio mambo ya teknolojia yanayofanya watu kutumia intaneti kufanya vitu vingi tuu ndani ya sekunde zipatazo sitini hivyo basi kuweza kufanikisha kile ambacho mtu ameaka kukifanya.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.