fbpx
Anga, NASA, Ndege, Ndege, Teknolojia, Usafiri

Stratolaunch: Ndege kubwa zaidi duniani yapaishwa nchini Marekani

stratolaunch-ndege-kubwa-zaidi-duniani
Sambaza

Kampuni ya Stratolaunch nchini Marekani imefanikisha majaribio ya kurusha ndege kubwa zaidi duniani kwa sasa. Ndege hii kutumika kwa ajili ya huduma za anga ya juu ya duniani kama vile uwekaji satelaiti.

Kampuni ya Stratolaunch ilianzishwa na marehemu Paul Allen, aliyekuwa mmoja wa waanzilishi wa Microsoft.

ndege kubwa
Kwa umbo hii ni moja ya ndege kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa

Kutoka upande mmoja wa bawa la ndege hiyo hadi upande mwingine ni urefu ulio sawa na urefu wa kiwanja cha mpira wa miguu. Pia ndege hiyo inaundwa na pande mbili zikiwa zote zina eneo la rubani ingawa itaitaji kuendeshwa kwa kutumia upande mmoja tuu.

Kwa haraka haraka umbo lake ni sawa na kuchukulia ndege mbili kuunganishwa ili kutengeneza moja.

INAYOHUSIANA  Yanayojulikana Kuhusiana Na Samsung Galaxy Note 8 Mpaka Sasa!
ndege kubwa duniani
Kwa ukaribu, upande mmoja wa ndege hiyo

Ndege hii ambayo imetengenezwa na kampuni ya Stratolaunch iliyoanza kazi zake mwaka 2011 inalenga kutoa huduma za kusafirisha rokoti kwenye anga za juu za dunia. Kwa kutumia ndege yenye uwezo wa kwenda na kurudi inategemewa kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa huduma za kurusha kupeleka satelaiti kwenye eneo la juu/nje ya dunia (orbit).

Sifa mbalimbali za ndege hii;

  • Ina injini 6 za urushaji ndege, 3 kila upande.
  • Ukubwa wa urefu kutoka upande mmoja wa bawa hadi mwingine ni mita 118
  • Eneo lake la kati kati litaweza kubeba roketi ambayo itaweza kuwashwa na kuachiwa anga za juu kabisa. Roketi ndio itaenda na kuweka satelaiti kisha yenyewe itaungua angani
  • Landing gears – mfumo wa matairi uliotumika unahusisha matairi yanayotumika kwenye ndege za familia ya Boeing 747 – ndege zenye sifa ya kuhimili uzito mkubwa
  • Ndege inauzito wa kilo 250,000, inaweza kurusha mzigo wa hadi kilo 240,000.
  • Kwa uwezo huu inategemewa itakuwa na uwezo wa kubeba hadi roketi tatu.
INAYOHUSIANA  Ijue Hot Knot; Sahau Kutuma Mafaili kwa Teknolojia ya Bluetooth, hii ni Bora Zaidi
ndege boeing 747
Mfumo wa matairi unahusisha kutumia mfumo wa ndege ya Boeing 747, ndege hii inamatoleo mawili – ya abiria na mizigo.

Kwa kutumia ndege hii inamaanisha gharama za zamani ambazo zilihusisha utengenezaji wa roketi ambazo ziligharimu pesa nyingi na huku zikitumika mara moja tuu – gharama hizi zitaokolewa.

Zamani na ata kwa sasa utumaji wa satelaiti kwenye anga za juu za dunia unahusisha utumiaji wa roketi kadhaa kwenye safari moja, kuna kuu zinazofanya kazi kuanzia mwanzo wa safari na kisha kuachwa zikidondoka na kuachia roketi zengine kuendelea na safari.

INAYOHUSIANA  Je, unajua kuwa Mkono 'huathiri' mawimbi ya simu? #Utafiti
stratolaunch
Picha ya mfano: Inaonesha roketi ikiwa eneo la kati kati kabla ya kuachiwa ili iendelee na safari huku ndege kuu ikirudi ardhini.

Majaribio haya ambayo bado ni endelevu na yatahusisha wiki hadi miezi kadhaa kabla ya kupata vibali vya kuruhusu ianze kutumika rasmi. Kwa sasa sifa ya ndege kubwa zaidi inashikiliwa na ndege ya mizigo ya Urusi ya Antonov An-225

Wateja wakuu katika huduma hizi ni pamoja na NASA (Shirika la tafiti za anga Marekani), makampuni ya biashara na mataifa yanayotaka kuweka satelaiti kama za uchunguzi wa hali ya hewa na teknolojia zingine za mawasiliano.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |