Ndugu na Marafiki sasa kupost kwenye akaunti za Marehemu Facebook kwa urahisi zaidi. Facebook kwa muda sasa wameweza kuziwekea vitu akaunti za watu waliofariki ili wengine kuweza kutambua kwa urahisi. Vitu hivyo ni pamoja na neno “REMEMBERING” ambalo linatambulisha kama mmiliki wa akaunti amefariki dunia.
Mbali na ilo Facebook sasa wameamuwa kuongeza sehemu ya “Tributes” ambayo itaweza kuwawezesha ndugu na marafiki kuweza kuandika kumbukumbu katika ukurasa wa marehemu.
Picha : Facebook
Pia mbali na hii Facebook wameongeza uwezo katika “LEGACY ACCOUNT” ambazo huchaguliwa na mtu kuweza kuiongoza akaunti yake endapo tu akifariki. Hii itafanya mtu ambaye umemchagua – ‘Legacy’ kuwa na uwezo wa kuiongoza akaunti yako ikitokea umefariki. Pia Facebook inawapa uwezo wa watu kutuma maombi ya kuiongoza akaunti ya marehemu.
Mbali na yote haya POSTS za marehemu zitabaki kuhifadhiwa kwa namna ambayo itakuwa vigumu watu kuona ili kuepusha ndugu kuwapa majonzi. Mambo mengine kama kupendekezwa kwa akaunti ya marehemu kwenye makundi ya Facebook na kuzuia akaunti za marehemu kutuma mialiko(invititions) kama ya birthdays kwa watu wengine. Haya yote yatasimamiwa na AI features za Facebook (Yaani akili kompyuta/feki).