fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Maujanja Teknolojia whatsapp WhatsApp Beta

Uwezo wa kukata sauti ya video kwenye WhatsApp. #Maujanja

Uwezo wa kukata sauti ya video kwenye WhatsApp. #Maujanja

Spread the love

Je, umeshawahi kutaka kukata sauti ya video kwenye WhatsApp kabla ya kutuma kwa mwingine/wengine? WhatsApp waleta uwezo huo.

Kwenye dunia ya leo WhatsApp imekuwa moja ya kiungo muhimu cha kufanikisha mawasiliano ya watu sehemu nyingi duniani na mara kwa mara imekuwa ikiboreshwa ili kuendana na kile kinachohitajika lakini pia kuzidi kuwavutia watu wengi zaidi.

Nikiwa kati ya watu wengi ambao wanatumia WhatsApp kama moja ya njia ya mawasiliano lakini ambae nilishawahi kutumia toleo la majaribio kwa muda mrefu tuu nimefurahishwa na hili la kwamba mtu kuwa na uwezo wa kuondoa sauti ya picha jongefu pale kabla ya kuwatumia/kuisambaza kwa wengine au kuiweka kwenye habari zake za siku hiyo (status).

Kwa mujibu wa taarifa WhatsApp Beta yoleo la karibuni kabisa tangu Feb 27 wamekutana na kipengele kipya ambapo mtu ana uwezo wa kutoa sauti kwenye picha mnato kabla ya kuisambaza/kuichapisha kwenye uwanja wake ili wengine waweze kuona.

kukata sauti

Uwezo wa kukata sauti ya picha jongefu kwenye WhatsApp kabla ya kuisambaza.

Mbali na hilo WhatsApp wameonekana wakienda mbele na kurudi nyuma kuhusu watumiaji wake kuweza kutumia akaunti zao za WhatsApp kwenye vifaa viwili tofauti kwa wakati huohuo ingawa kipengele hicho si kipya kwani kimekuwa kikiletwa na kuondolewa kwa mara kadhaa sasa. Na kwa mujibu wa WhatsApp Beta toleo 2.21.30.16 inaruhusu mtu kuweza kufunga (log out) moja ya akaunti yake ambayo imeunganishwa sehemu nyingine.

SOMA PIA  Fanya Kivinjari Cha EDGE Kufuta Taarifa NYETI Za Kimtandao Pale Unapokifunga!

Hivi sasa maboresho hayo yanapatikana kwa wanaotumia WhatsApp Beta tu. Bado haijajulikana ni lini maboresho hayo yatapatikana kwa watumiaji wote wa WhatsApp wakimemo wanaotumia iOS. Unaizungumziaje habari hii?

Vyanzo: Gadgets 360, WaBetaInfo

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. Dickson Munis - March 9, 2021 at 10:17 - Reply

    Nmependa habar zako upo makin san pongez

  2. […] WhatsApp programu tumishi inayotumiwa na watu wengi zaidi duniani kama njia ya kufanya mawasiliano kila mara inaboreshwa na sasa umesikia hii ya uwezekano wa kuhamisha mazungumzo yako kwenda namba nyingine? […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania