fbpx

Utafiti: iPhone ni za wanawake masikini, Huawei ni kwa wanaume wenye nazo!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Utafiti wa hivi majuzi umetoa matokeo ya kushangaza baada ya kubaini kuwa wengi wa watumiaji wa simu za iPhone huwa masikini, huku mabwenyenye wakisemekana kupendelea simu za Huawei.

Utafiti huo wa kampuni moja kutoka Uchina kwa jina MobData ulifanywa miongoni mwa watumiaji wa simu janja  nchini humo (Uchina).

Kwa mujibu wa MobData, kuwa watumiaji wengi wa simu za iPhone ni wale wa mapato ya chini na wa kawaida ambao walitajwa kuwa ‘Watu masikini wanaotaka kujionyesha kuwa wenye pesa’.

Vilevile, utafiti ulisema kuwa wengi wa watu wanaopendelea simu za iPhone ni wanawake wasio na wapenzi wa kati ya umri wa miaka 18 na 34, ambao mapato yao ni ya chini na pia walio na elimu ya kiwango cha chini ikilinganishwa na watumiaji wa aina nyingine za simu.utafiti

Utafiti huo aidha ulidhihirisha kuwa watumiaji wa simu za Apple hawana hulka ya kuhamahama kununua aina nyingine za simu, ukisema kuwa asilimia 65.7 ya watumiaji wa simu hizo watanunua aina hiyo tu wakati wanapoamua kununua simu mpya.

Watumiaji wa Huawei nao walisemekana kuwa wanaume walio katika ndoa na kati ya umri wa miaka 25 na 34. Wengi wao wanapata mshahara mnono wakilinganishwa na wale wanaotumia iPhone na ni wafanyakazi wa taaluma fulani ama kazi zisizo za taaluma.

utafiti

Kulingana na utafiti wanaotumia Huawei wengi wao ni wafanyabiashara waliofanikiwa maishani.

Haya sasa wewe kama mtu unayetumia simu janja za Huawei/iPhone una lipi la kusema? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Matumizi ya simu jela: Simu 13,000 zakamatwa Uingereza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.