fbpx
Apple, IPhone, simu

Ujio wa iPhone 9 ni kitendawili

ujio-wa-iphone-9-ni-kitendawili
Sambaza

Mwaka huu Apple walitegemewa kutoa toleo la iPhone 9 lakini suala hilo limegeuka kuwa kitendawili kutokana na sababu mbalimbali ambazo imewabidi tuu wasubiri kwanza ila haijulikani mpaka lini.

Mataifa mengi hivi sasa yanapambana na virusi hatari vya Corona jambo ambalo limesitisha shughuli nyingi tuu za kiuchumi, siasa na kijamii ili kuweza kupungnuza uwezekano wa janga hilo kuwapata watu wengi na hivyo basi kupoteza nguvu kazi. Katika siku za usoni kampuni hiyo ilitarajiwa kufanya mkutano wake na wataalamu wa kuunda (Worldwide Developer Conference [WWDC]) ambapo ndipo ilitegemewa kuzinduliwa kwa simu hiyo pamoja na bidhaa nyingine.

INAYOHUSIANA  Simu Janja 5 Zinazosubiriwa Kwa Hamu!

iPhone 9 ni simu inayotegemea kuja kuinua mauzo ya Apple kwa mwaka huu ikitabiriwa kuwa itanunulika kwa wingi kwa sababu ni simu ya uwezo wa kati na hata bei yake haitakuwa ghali kama matoleo mengine ambayo yapo sokoni tayari. Hivi sasa nguli hao kwenye biashara wapo kwenye kipindi kigumu katyika upatikanaji wa mapato hasa nchini Uchina ambapo CoVID-19 ndipo ilianzia.

kitendawili
iPhone 9 ama wengine wakisema ni iPhone SE 2 lakini sasa imebaki kuwa kitendawili kuhusu ujio wake.

Tofauti na iPhone 9 Apple pia kuna toleo jipya la iPad Pro ambayo inaelezwa itakuwa na maboresho makubwa kwenye kamera na teknolojia ya 3D ToF. Mkutano wa WWDC umesogezwa mbele hadi mwezi Juni na utafanyika msaada wa TEHAMA (mtandaoni na kila mtu akiwa sehemu yake).

Vyanzo: Forbes, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|