fbpx

M-Pesa kutuma fedha kwenda Uchina kupitia WeChat

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Watumiaji wa M-Pesa kupitia mtandao wa Safaricom nchini Kenya sasa wana uwezo wa kutuma mara moja kwa moja kwenda Uchina kupitia mtandao wa kijamii wa WeChat.

Hilo limewezeshwa kwa ushirikiano kati ya benki ya Family na kampuni ya iliyopo London, SimbaPay itawawezesha watumiaji wa M-Pesa takribani 23,946,174 nchini Kenya kutuma fedha kwa watuamiaji wa WeChat ambao ni zaidi ya bilioni 1 nchini Uchina.

Namna ya kutuma fedha, Wakenya watatumia nambari ya malipo ya M-Pesa ya Benki ya Familia (Family Bank) na kuweka namba ya simu ya mpokeaji nchini Uchina kama nambari ya akaunti.

kutuma fedha

Gharama ya kutuma italiangana na kiwango cha fedha kitakachotumwa mathalani kutuma $80 itakatwa shilingi 350 ya Kenya.

Mbali na M-Pesa, wateja wa Benki ya Familia pia watatuma fedha kwa watu wa Uchina kwa WeChat kupitia programu ya benki ya PesaPap ya benki na huduma ya USSD.

INAYOHUSIANA  Uchina: App kukutaarifu watu wenye madeni ya mikopo benki wakiwa karibu yako

Wateja watapokea taarifa ya papo hapo kuwajulisha kiasi ambacho watatuma kwa shillingi ya Kenya, na kiwango cha ubadilishaji wa fedha ya Uchina (Yuan) ambacho mpokeaji atapata.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.