fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Asus simu Teknolojia Uchambuzi

Undani wa kina kuhusu Asus Zenfone 8 Flip

Undani wa kina kuhusu Asus Zenfone 8 Flip

Spread the love

Katika simu janja ambazo zinavutia kwa macho lakini hata undani wa rununu yenyewe basi Asus wanafanya kweli kuweza kuvutia wateja sehemu nyingi duniani.

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa makala za TeknoKona kwa muda mrefu tuu kabla na baada ya kujiunga nao leo hii ikanibidi nikae chini kuandaa undani wa sifa za rununu Asus Zenfone 8 Flip ambayo imesheheni sifa lukuki kipengele baada ya kipengele. Si vifaya na wewe ukasoma hakala hii hadi mwisho.

Urefu wa kioo|Kipuri mama

Kwa yeyote anayejua kuchagua simu janja nzuri atazingatia toleo/aina ya kipuri mama ambacho kimewekwa humo ili kuifanya rununu husika kuwa na uwezo mkubwa wa kukamilisha kazi zake. Asus wameweka Snapdragon 888 5G kwenye simu husika. Kioo ni Gorilla Glass 6 mbele, nyuma-Gorilla Glass 3 ikiwa na uzio wa alminium, kina ung’avu wa hali ya juu (Super AMOLED ya Samsung), chenye urefu wa inchi 6.67 (1080x2400px, 90Hz).

 Zenfone 8 Flip

Uso wa mbele wa Asus Zenfone 8 Flip.

Diski uhifadhi|RAM

Kipengele kingine ambacho watu wengi duniani kote wanakizingatia wakati wa kufanya maamuzi ya kununua simu janja ni upande wa memori na kimsingi wameweka nguvu ya kutosha hapa kwani kuna GB 8 RAM kwa GB 128/256GB za diski uhifadhi lakini pia ikiwa na nafasi ya kuweka memori ya ziada mpaka TB 2.

SOMA PIA  Morogoro: Drones kusaidia kutatua migogoro ya ardhi

Kamera|Betri

Macho ya wateja wengi duniani pia hutolea macho uwezo wa kamera lakini pia nguvu ya betri, toleo la Zenfone 8 Flip lina 5000mAh (siku 2 bila kuichaji, saa 9.8 za kuperuzi kwa kasi ya 5G, saa 19 za kama utaitumia kwa kuangalia picha za mnato tu ama siku 12.4 kama itakuwa imewashwa pekee), nguvu ya kuchaji haraka kwa 30W. Kwenye kamera simu hiyo ina kamera tatu tu zenye MP 64, MP 12 na MP 8, ndipo hapa palipobeba sehemu ya jina la rununu-flip likiwa na maana ya uwezo wa kuzipundua na kuwa kamera ya nyuma au mbele halikadhalika taa ya kuongeza mwangaza ipo pia.

 Zenfone 8 Flip

Simu hii yenye kamera zilizotengenezwa na Sony zina uwezo wa kuchukua picha jongefu zenye ubora wa 8K, 4K, 1080px na 720px lakini uwezo wa kupata picha kwenye nyuzi 112.

Bei|Mengineyo

Simu hiyo inatumia ZenUI 8, Android 11, uzito wake ni gramu 230, WiFi 6E, Bluetooth 5.2, inatumia kadi mbili za simu, teknolojia ya kuchaji ni USB-C, USB Power Delivery 3.0, usalama wa kutumia alama ya kidole upo ndani ya kioo, Google Assistant, NFC vipo, inatumia 5G. Bei ya 8/256GB ni $969|zaidi ya Tsh. 2,230,149 kwa ughaibuni.

 Zenfone 8 Flip

Ndani ya boksi utakutana na mfuko wa kuzuia madhara/michubuko kwenye rununu, kichwa cha chaji, waya wa kuchajia, kipini cha kutolea kadi ya simu na simu yenyewe kulingana na rangi ambayo utakuwa umeichagua-Nyeusi ama Fedha.

Simu hiyo upatikanaji wake kwa sasa ni kwa kuiagiza hivyo basi hatuna budi kuwa na subira kuisubiri ifike kwetu. Nini maoni yako kuhusu simu hiyo? Usiache kufuatilia TeknoKona kila leo!.

Vyanzo: Asus, GSMArena

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania