Microsoft watambulisha laptop mpya na simu ya kiutofauti. #Uchambuzi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Microsoft watambulisha laptop na tableti mpya kadhaa. Kampuni ya Microsoft imetambulisha bidhaa mpya kadhaa ambazo zinaonesha kwa kiasi gani kampuni hiyo inazidi kuwa ya kibunifu kwenye bidhaa zake mpya.

Bidhaa hizo zinaongeza idadi ya bidhaa zinazopatikana katika familia ya bidhaa za Microsoft zinazobeba jina la Surface.

Surface Laptop 3

Toleo jipya la laptop ya Surface linalotambulika kama Surface Laptop 3 ni laptop inayokuja na kioo/display inayotambua miguso ya vidole (touchscreen). Laptop hii inakuja katika ukubwa wa inchi 13 na 15. Mkurugenzi wa kitengo cha bidhaa/devices, Bwana Panos Panay amesema laptop hizi zina kasi ya ufanisi wa hadi mara tatu ukilinganisha na laptop za MacBook Air zinazotengenezwa na Apple.

Surface Laptop 3 Microsoft watambulisha laptop mpya

Surface Laptop 3: Microsoft watambulisha laptop mpya

Sifa zake;

 • Uwezo wa kuchaji wa haraka – hadi asimilia 80 ndani ya lisaa limoja
 • Prosesa ya Intel ikiwa inaambatatishwa na kadi za graphic za AMD.
 • Kingine kizuri kwenye laptop hizi ni urahisi wa kufanya matengenezo au kubadilisha vipuri vya ndani. Microsoft wamerahisisha uwezo wa kuifungua na kupadilisha vitu kama diski na vinginevyo.

Surface Laptop 3 zitapatikana kwa bei ya $999 na $1,199 na zitaanza kupatikana mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Surface Pro 7

Tablet za Surface zimeanza kujipatia umaarufu sana kwa uwezo wake wa kutumika kwa kazi nyingi ambazo kikawaida huwa zinafanyika kwenye kompyuta/laptop.

INAYOHUSIANA  Netflix ya Magemu? Microsoft waja na huduma ya malipo ya mwezi, magemu 100+

surface pro 7 Microsoft watambulisha laptop mpya

Pro 7 ni toleo jipya la tableti za uwezo wa juu kutoka Microsoft zinazobebaga jina la ‘Surface Pro’. Hizi ni tableti zenye uwezo mkubwa wa kikompyuta zinazokuja na toleo la Windows 10.

Uwezo wake;

 • Inakuja na teknolojia ya USB-C na USB-A.
 • Ukubwa wa inchi 12.3
 • RAM: Matoleo ya GB 4, GB 8 au GB 16
 • Uzito wa gramu 771.1
 • Diski ujazo: Kuna matoleo ya aina nne, GB 128, GB 256, GB 512 au TB 1 (Zote mfumo wa SSD).
 • Betri: Uwezo wa hadi masaa 10.5 ya utumiaji
 • Prosesa aina 3: Dual-core 10th Gen Intel® Core™ i3-1005G1 Processor, Quad-core 10th Gen Intel® Core™ i5-1035G4 Processor, Quad-core 10th Gen Intel® Core™ i7-1065G7 Processor

Surface Pro 7 itaanza kupatikana Oktoba 22 mwaka huu. Bei inaanza kwa $749.00 (Tsh 1,716,558.20).

Surface Pro X

Kutoka toleo la Surface Pro 7, Microsoft wameleta pia toleo la Surface Pro X. Tableti hii yenye uwezo wa kutumia keyboard za mpachiko, inakuja na prosesa ya kisasa aina ya Snapdragron kutoka Qualcomm. Inakuja na uwezo wa kutumia teknolojia ya kisasa ya LTE kupitia uwezo wa kuwa na laini ya simu ndani yake.

INAYOHUSIANA  Uchambuzi wa simu ya Tecno Phantom 9 (Video)

Surface Pro X Microsoft watambulisha laptop mpya

Sifa zingine;

 • Ukubwa wa display wa inchi 13
 • Inawembamba wa mm 5.33 na uzito wa takribani gramu 762
 • Inakuja na port za USB-C mbili
 • Betri: Uwezo wa kukaa na chaji wa kufikia masaa 13 ya utumiaji
 • Ujazo: Diski za SSD zinazoweza kutolewa kwa urahisi – GB 128, GB 256 au GB 512.
 • Inasehemu ya kuweka SIM ya mfumo wa Nano na ikiwa na uwezo wa LTE (4G)
 • Prosesa na Graphics zimetumika za Microsoft;Microsoft® SQ1™ Adreno™ 685 GPU

Keyboard yake ambaye inauzwa kama kifaa cha ziada ina uwezo wa kuchaji peni spesheli ya kutumia kwenye tableti (stylus)

Tofauti na keyboard zingine za tableti hasa hasa zile za Apple keyboard hii inakuja na eneo la mouse (touchpad).

Surface Pro X itaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi Novemba kwa bei ya $999 (Takribani Tsh 2,289,508.20 )

Surface Neo

Surface Neo ni laptop ya kiana yake. Ni laptop inayofunguka kama kitabu na huku pande zote zikiwa na display ya mfumo wa mguso (touchscreen).

Microsoft surface neo

Surface Neo

Ina wembamba wa mm 5.6 na uwezo wa kukunjuka hadi kufikia nyuzi 360 – yaani unaweza kukunja kwa kufunga au kufungua hadi mwisho. Peni spesheli, stylus, inaweza kugundishwa kwa nyuma – kwa mfumo wa sumaku na kuweza kupata chaji moja kwa moja kutoka kwenye laptop hii kwa njia ya ‘wireless’.

Mnunuaji ataweza pia kununua keyboard ya pembeni, ambayo pia inauwezo wa kuwekwa juu ya kioo/display moja wapo na kutumika kama kawaida. Ni keyboard inayokuja kwa mfumo wa bluetooth.

Surface Neo  Microsoft watambulisha laptop mpya

Surface Neo: Keyboard ikipachikwa upande mmoja

Usitegemee Surface Neo mwaka huu, Microsoft wamesema wanataka kuhakikisha laptop hii itakapoingia sokoni iingie ikiwa katika ubora mzuri na hivyo wanategemea upatikanaji wake kuwa mwishoni wa mwaka 2020.

INAYOHUSIANA  Huawei Y360, Kiki Inayopewa Inafanana na Ubora wa Simu Husika?

Surface Duo

Bidhaa nyingine ambayo imetambulishwa ila usitegemee kuiona hivi karibuni sokoni ni simu-tableti ya kitofauti inayokwenda kwa jina la Surface Duo.

Surface Duo

Surface Duo

Ni simu janja inayokuja na programu endeshaji ya Android na ikiwa na sifa ya kuweza kufunguka kama vile ilivyo laptop ya Surface Neo.

Microsoft wamefanikiwa kutengeneza muunganisho wa ubora mzuri kuhakikisha hawatakutana na changamoto za kuharibika kwa display kama vile simu zingine mpya za mkunjo kutoka Samsung – Galaxy Fold au Huawei – Mate X.

Simu hii wamesema bado ipo kwenye maboresho zaidi na hivyo itegemewe mwakani mwishoni.

Vipi una mtazamo gani juu ya bidhaa hizi kutoka Microsoft? Ni bidhaa ipi iliyokuvutia zaidi?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.