Lenovo wamezindua simu yao ya Lenovo Moto X Force ambayo ni simu yenye uwezo wa kuhimili vishindo bila kuvunjika, simu hii haitavunjika kioo pindi itakapoanguka zaidi labda inaweza kupata mkwaruzo pembeni.
Simu hii itakufanya usihitaji kabisa kava la simu kabisa na kama unamtoto mdogo basi hutahitaji kuificha simu yako kuogopa ataivunja.
Teknolojia nyuma ya muundo wa simu hii
Simu hii imetengenezwa pamoja na teknolojia ya ShatterShield ambayo watengenezaji hawa wanadai kwamba inahusisha kioo ambacho kina safu tano ambazo zimetengenezwa mahususi kuzuia kioo kuvunjika pindi simu inapoanguka.
Safu ya kwanza inakuja na uwezo wa kuhimili michubuko hii ina maana kwamba simu yako haitahitaji tena screen protector, na zaidi ya yote kioo cha simu hii kitakuwa na safu mbili (yaani safu ya pili na ya tatu)kwaajiri ya touch screen ambayo moja ni ya akiba kama itatokea moja itakufa.
Safu ya nne ya ni AMOLED kioo’ ambacho pamoja na mambo yote kina uwezo wa kuhimili mshindo.
Simu hii imepata majaribio mengi, watu wengi wamerekodi video wakiiangusha kushindanisha na simy nyingine maarufu kama iPhone na Samsung ha imeoesha kwamba inaweza kuhimili vishindo ingawa katika uzinduzi wa simu hiyo huko India simu ilipata crack kidogo hasa katika body ya simu.
Hapo juu ni moja ya video ambayo inaonesha simu hiyo ikidondoshwa katika kima sawa na simu nyingine mbili za iPhone na Samsung ambazo zinavunjika.
No Comment! Be the first one.