fbpx

Huawei, simu, Uchambuzi

Ifahamu simu ya Huawei Mate X, simu nyingine ya mkunjo. #Uchambuzi

sasa-ni-rasmi-kuhusu-huawei-mate-x

Sambaza

Siku ya leo (Feb 24) huko Barcelona-Uhispania limefanyika onyesho kubwa la bidhaa za kidijiti na makampuni mbalimbali yameweza kuzindua vitu mbalimbali mojawapo ni Huawei Mate X.

Kwa muda sasa palikuwepo fununu kuhusu sifa/undani wa simu janja vinayokwenda kwa jina la Huawei Mate X na hii inatokana hasa kuwa ni simu janja ya kwanza kutoka kwao inayojikunja lakini pia ikiwa toleo lao la kwanza lililowekewa teknolojia ya 5G.

Yale yote ambayo tulikuwa tunayosoma kupitia toviti mbalimbali sasa tuweke pembeni tuweke kujua simu husika ina uzuri gani mbali na ambavyo tumekwishavidokeza?

>Uwezo wa betri

Betri ya kwenye simu hiyo ina 4500mAh na pia imewekwa teknolojia ya kuweza kuchaji haraka 55W; inachukua nusu saa tu kufikisha 85% ya umeme ulioingia kwenye betri.

>Muonekano

Ni simu ambayo ina uwezo wa kukunjika/kukunjuka hivyo basi ikiwa imekunjuliwa inakuwa tabiti ya kioo cha incihi 8 na ung’avu wa kioo ni  2480 x 2200 pixels. Pale ambapo kioo chake kinakuwa kimekunjwa ni urefu wa inchi 6.4 upande mmoja na mwingine unakuwa na inchi 6.6.

SOMA PIA  Je, Urefu Wa Chaja Unaathiri Kiwango Cha Chaji Inayoingia Katika Kifaa Chako?

>Kipuri mama/Rangi

Ufanisi wa simu unategemea sana nguvu ambayo imewezesha nikimaanisha kipuri kinachofanikisha kzi zote. Huawei Mate X imewekwa Kirin 980. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali simu hiyo itakuwa ikipatikana katika rangi moja tu-Bluu

>RAM/Diski uhifadhi+Menginyo

Simu hiyo inayojikunja kutoka Huawei ina RAM ya GB 8, GB 512 upande wa diski uhifadhi. Sehemu ya kuchajia ya teknolojia ya USB-C, inatumia kadi mbili za simu, sehemu ya teknolojia ya alama ya kidole ndio hapohapo mahali pa kuzima/kuwasha simu. Vilevile, haina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni.

SOMA PIA  Vifaa Vya Muhimu Vya Kuwa Navyo Kwa Ajili Ya Simu Janja Yako!
Huawei Mate X
Sifa za kamera hazijajulikana lakini pande zote mbili (ikiwa imekunjwa) zina kamera na kwa pembeni kuna kaera 3 zilizojificha.

Huawei Mate X inaelezwa kuwa ndio simu janja ianyojikunja ya kwaza kabisa nyembamba zaidi (11mm), bei yake ni $2,600|Tsh. 5,980,000 na itaanza kupatikana (kuuzwa) mwezi Juni 2019.

Vyanzo: GSMArena, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

    1 Comments

    1. Tuendelee tuu kusubiri kuhusu Mate X kuingia sokoni -
      July 29, 2019 at 1:35 am

      […] ya simu zinazokunjika imerudi tena machoni pa watu na moja ya rununu ambazo zinauwezo huo ni Huawei Mate X lakini ipo wazi kabisa kuwa kampuni husika imekumbana na changamoto nyingi ambazo zimesababisha […]