Samsung wafunga kiwanda nchini China

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Samsung wafunga kiwanda nchini China. Kampuni hiyo inayoshikilia namba moja katika utengenezaji na uuzaji wa simu janja duniani, imefunga kiwanda chao pekee nchini China kwa ajili ya utengenezaji wa simu.

Katika taarifa walioiweka wazi jumatato hii kampuni hiyo imesema imefikia uamuzi wa kufunga kiwanda hicho ili kuendana na hali ya uhitaji.

Samsung wafunga kiwanda China

Samsung wafunga kiwanda China: Kwa sasa kampuni hiyo inakuwa bila kiwanda cha simu janja nchini humo.

Kwa kifupi kwa muda mrefu kampuni ya Samsung imejikuta ikiporomoka katika soko la simu janja nchini humo.

INAYOHUSIANA  Je Unataka Kuamka? Fahamu kengele bomba kwa Android!

Kwa mahitaji ya simu janja zenye ubora watu wengi ununua simu kutoka kampuni ya Huawei na Xiaomi. Pale wanapohitaji simu za bei ya juu basi huwa wananunua simu za daraja la juu za Huawei na pia iPhone kutoka Apple. Simu za Samsung zimekuwa haziuziki kwa kasi kama zamani.

Nafasi ya simu za Samsung katika soko la simu janja nchini China imeporomoka kutoka umiliki wa asilimia 15 katikati ya mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 1 mwanzoni mwa mwaka huu.

INAYOHUSIANA  RIM Yazidi Kuyumba. Simu za Blackberry 10 Hadi Mwakani!

Kiwanda hichi kinachofunga kilikuwa kinafanya kazi tokea mwaka 1992 na inakadiriwa kuna wafanyakazi 6,000 watakaokuwa wameathirika na uamuzi huu. Mwaka 2017 kiwanda hicho kilikuwa na uwezo wa kutengeneza simu milioni 63 kwa mwaka.

Kwa sasa kwa makampuni makubwa ya kigeni Apple tuu ndio atakuwa bado amebaki katika utengenezaji wa bidhaa zake nchini humo. Samsung amekeza zaidi katika viwanda vya gharama nafuu za uendeshaji katika mataifa ya India na Vietnam katika miaka hii ya karibuni.

samsung wafunga kiwanda China

Samsung wamekuwa wakihamishia viwanda vyake katika mataifa ambayo wanafanya vizuri kimauzo na pia kwenye gharama nafuu za uendeshaji, hii ni pamoja na India na Taiwan

Ingawa wanaondoa kiwanda chao nchini humo bado Samsung wamesema wataendelea kuuza simu janja zao katika taifa hilo.

Vyanzo: Yahoo na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.