fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Asus simu Teknolojia

Zifahamu Asus Zenfone 7 na 7 Pro

Zifahamu Asus Zenfone 7 na 7 Pro

Ukiwa ni mtu unayependa kununua kitu kizuri hasa kwa kutaka kuchagua simu janja kwa jicho la karibu zaidi inawezekana kabisa ukapata wakati mgumu wa kutaka kuchukua simu ipi hasa hizi ambazo zinatumia Android.

Wakati fulani huko nyuma nilishawahi kuandika makala kuhusu Asus Zenfone 6 ambayo ina upekee wa aina yake uliolivutia jicho langu. Jicho langu tena limetokea kuvutiwa na Asus Zenfone 7 halikadhalika 7 Pro ambazo zipo sokoni kwa miezi kadhaa sasa. Je, unafahamu sifa zake?

Sifa za Asus Zenfone 7

Memori :
 • Diski uhifadhi: 128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka TB 2
 • RAM: 6GB/GB 8
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 64, 12, na 8+taa mbili za kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu
 • Kamera ya Mbele: kamera za nyuma ndio hizo hizo za mbele maana yake ni zinaonekana kwa mtindo wa kufunua na kufunika
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB-C+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 30W (60% kwa dakika 34 na kufika 100% inachukua dakika 93)
Kipuri mama :
 • Snapdragon 865 5G

Programu Endeshi

 • Zen UI 7, Android 10 ingawa sasa imewezeshwa kwenda Android 11 tangu mwezi Machi
Rangi/Bei :
 • Nyeusi na Nyeupe
 • GB 6/128-$542 (zaidi ya Tsh. 1,246,600) na GB 8/128-$609 (zaidi ya Tsh. 1,400,700) bei ya ughaibuni
  Zenfone 7

  Asus Zenfone 7 ina teknolojia ya 5G, Bluetooth 5.1, NFC, inatumia kadi mbili za simu, haina sehemu ya kuchomeka spika za masikoni, ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole.

Sifa za Asus Zenfone 7 Pro

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.67 (1080×2400 px)
 • Ubora: Super AMOLED, ung’avu wa hali ya juu sana/Gorilla Glass 6 kwa mbele na Gorilla Glass 3 uso wa nyuma
Memori :
 • Diski uhifadhi: 256GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada mpaka TB 2
 • RAM: GB 8
Kamera :
 • Kamera Kuu: MP 64, 12, na 8+taa mbili za kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu
 • Kamera ya Mbele: kamera za nyuma ndio hizo hizo za mbele maana yake ni zinaonekana kwa mtindo wa kufunua na kufunika
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB-C+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 30W (60% kwa dakika 34 na kufika 100% inachukua dakika 93)
Kipuri mama :
 • Snapdragon 865 5G+

Programu Endeshi

 • Zen UI 7, Android 10 ingawa sasa imewezeshwa kwenda Android 11 tangu mwezi Machi
Rangi/Bei :
 • Nyeusi na Nyeupe
 • GB 8/256-$799 (zaidi ya Tsh. 1,837,700) bei ya ughaibuni
  Zenfone 7

  Asus Zenfone 7 ina teknolojia ya 5G, Bluetooth 5.1, NFC, inatumia kadi mbili za simu, haina sehemu ya kuchomeka spika za masikoni, ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole.

TeknoKona tumekamilisha kazi yetu ya kuleta mbele ya macho yako rununu mbili ambazo kwa hakika zinafutia katika ulimwengu huu wa kisasa. usisite kutuandikia maoni yako kuhusu makala hii na daima usiache kutufuatilia kila iitwapo leo.

Vyanzo: GSMArena, Mr. Phone, Gadgets 360

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania