Kwa miaka mingi tuu watumiaji wa Twitter kwenye Android wamekuwa wakikikosa kisanduku cha kuweza kutafuta jumbe ndani ya uwanja husika lakini hilo sasa limefikia tamati.
Kwa karibu miaka miwili sasa Twitter upande wa iOS wamekuwa wakipata wepesi wa kuweza kufikia jumbe mbalimbali kiurahisi na hii imetokana na uwepo wa sehemu mahususi ambayo imekuwa ikimuwezesha mtumiaji kutafuta jumbe kwenye kisanduku.
Katika maboresho ya hivi karibuni yaliyofanywa kwenye programu tumishi-Twitter upande wa Android sasa watumiaji wake nao pia wanaweza kufurahia maboresho hayo wakati hasa kwa yeyote ambae hapendi kutumia muda mrefu kutafuta kitu wakati wa kuperuzi huku na kule.

Mambo mazuri hayajaishia hapo kwani bado watumiaji wa Twitter wataweza kutafuta kitu mahususi kabisa mfano: mtu akikuandikia “Habari kaka….?” basi mtumiaji ataweza kutafuta ujumbe husika kwa kuutafuta kiurahisi akiamua kuandika herufi za mwanzo/katikati mathalani “Kak….” au “Hab…….“. Imeelezwea kipengele hicho kitaongezwa mwaka huu!.

hakika kwa haya maboresho yameletwa furaha kwa watumiaji wa Twitter upande wa Android ambao walisubiri kwa muda mrefu tuu tofauti na wanaotumia iOS. Je, wewe msomaji wetu umefurahishwa na habari hii? Tupe maoni yako na usisite kuwashirikisha wengine nao pia waweze kuhabarika.
Vyanzo: The Verge, Twitter
2 Comments