fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
instagram Kompyuta Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Instagram: Kuhusu kupandisha machapisho kupitia tovuti

Instagram: Kuhusu kupandisha machapisho kupitia tovuti
Spread the love

Licha ya watumiaji wengi wa Instagram ni wenye simu janja lakini wapo ambao kutokana na sababu mbalimbali kuna wakati wanatembelea akaunti zao kupitia tovuti (instagram.com) hasa kwa kutumia kompyuta.

Kuna vingi ambavyo haviwezekani kufanyika kwenye Instagram ukiingia kwenye akaunti yako kupitia tovuti lakini mtumiaji anaweza akajibu jibu jumbe, akaonyesha kupenda chapisho fulani, kutoa maoni yake kuhusu kitu fulani kwa kile kile kilichopandishwa na mtu.

SOMA PIA  WellPaper: Badili muonekano wa simu janja kulingana na matumizi

Utakubaliana na mimi kuwa ni muda mrefu watumiaji wa Instagram kuptia tovuti wamekuwa wakiakosa vitu vya muhimu ambayo vinawezekana kufanyika kupitia programu tumishi. Kuna habari njema ambapo Instagram upande wa tovuti inaboreshwa kiasi kwamba mtumiaji ataweza kupandisha machapisho kupitia tovuti ama kwa lugha rahisi “Kwa kutumia kompyuta“.

kupandisha machapisho

Kuhusu uwezekano wa kupandisha machapisho kwenye akaunti ya Instagram kwa kutumia kompyuta.

Katika maboresho hayo pia mtumiaji atakuwa na uwezo wa kuhamisha kitu anachotaka kukipandisha kwenye akaunti yake kiurahisi kwa kukivuta tuu kutoka sehemu kilipo mpaka pale amabpo kinatakiwa kuwekwa. Pia, itawezekana kufanya marekebisho kama ya kupunguza ukubwa wa chapisho, kuweka nakshi nakshi, kuwataja watu, kutaja mahali (nchi, mkoa, hoteli, n.k).

kupandisha machapisho

Mfano wa uwanja wa sehemu ya kufanya chapisho la Instagram liwe vizuri zaidi kupitia kompyuta kabla ya kwenda hewani.

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba maboresho hayo (kupandisha machapisho kwa kupitia tovuti) yanafanyiwa majaribio ndani kwa ndani na haijafahamika ni lini vitu hivyo vipya vitapatikana kwa walengwa ili hatimae kufanya utumiaji wa Instagram kompyuta uvutie.

Vyanzo: GizChina, GSMArena

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania