Serikali ya Uingereza yatishia kufungia mitandao ya kijamii

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Serikali ya Uingereza imetishia kufungia mitandao ya kijamii kupitia kampuni zao ikiwa hazitatoa jumbe ambazo zinazoweza kuwa hatari kiafya.

Waziri wa Afya Uingereza, Bw. Andrew Marr ameeleza kuwa kampuni hizo zisipokufuata maagizo ya serikali, sheria itapitishwa kuzipiga marufuku na pengine hata itungwe sheria itakayowezesha jambo hilo kuwa na nguvu zaidi.

Lengo la serikali ya Uingereza ni kushirikiana na makampuni yanayomiliki mitandao ya kijamii kuweza kuondoa jumbe ambazo zinaweza kusababisha watu kujiumiza/kujiua.

Msichana Molly Russel wa miaka 14 alijitoa uhai mnamo 2017 baada ya kutazama ujumbe uliomsumbua kuhusu kujiua. Baba yake mtoto huyo alieleza kuwa anaamini mtandao wa Instagram, chapisho kwenye Pinterest vilichangia mwanae kujiua.

kufungia mitandao ya kijamii

Kuhusu kufungia mitandao ya kijamii: Instagram ilikiri kuwa huwa hauondoi machapisho fulani ambayo yanaweza kuleta madhara kwa watu wengine wanapoyaona. Mtandao wa kijamii, Facebook nao uliomba msamaha kwa hilo, kwani ndio unamiliki Instagram.

Waziri huyo ameandika barua Twitter, Snapchat, Pinterest, Apple, Google na Facebook akipongeza hatua ambazo tayari zimechukua, na kutaka zizidi kuchukua nyingine zaidi.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Taarifa za mitandao ya kijamii ya Wachina wanaoingia Marekani kuangaliwa
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.