fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Apple Intaneti simu Teknolojia Uchambuzi

Prosesa za Simu janja zenye nguvu kuliko zote kwa mwaka 2021

Prosesa za Simu janja zenye nguvu kuliko zote kwa mwaka 2021
Spread the love

Unazifahamu prosesa za simu janja zenye nguvu kuliko zote? Teknokona leo tumekuandalia orodha ya prosesa 5 zenye nguvu kuliko zote pamoja na simu janja zinazotumia prosesa hizo. Kuna makampuni mengi duniani yanayotengeneza prosesa hizi ikiwemo kampuni ya Apple na Samsung.

Prosesa ni kichakataji kinachoiwezesha kompyuta kufanya mahesabu na maagizo mengine ya kimsingi ambayo hupitishwa kutoka kwenye mfumo wa uendeshaji (OS). Uwezo wa kompyuta au simu janja hutegemeana na uwezo wa prosesa kufanya kazi.

Aina 5 za prosesa za simu janja zenye nguvu ni:

SOMA PIA  BlackBerry Evolve na Evolve X zazinduliwa

Apple A15 Bionic; Prosesa hii hutengenezwa na kampuni ya Apple kwaajili ya simu janja zake na imetumika katika simu janja ya iPhone 13, iPhone 13 Pro, iPhone 13 Pro Max, iPhone 13 Mini na iPad Mini 2021. Prosesa hii ina spidi ya 3.23 GHz.

Prosesa za Simu janja

Picha: Muonekano wa Prosesa ya A15

Apple A14 Bionic; Hii pia ni prosesa iliyotengenezwa na kampuni ya Apple ambayo inatumika katika simu janja ya iPhone 12, iPhone 12 Pro, iPhone 12 Pro Max, iPhone 12 Mini na iPad Air. Prosesa hii ina spidi ya 3.1 GHz.

SOMA PIA  Muhstakabali wa kuona BURE chaneli za ndani

Snapdragon 888 Plus; Snapdragon ni kampuni kubwa ya kiteknolojia inayojihusisha na utengenezaji wa prosesa za simu janja pamoja na vifaa vingine vya kiteknolojia. Simu janja inayotumia prosesa hii Asus ROG Phone 5S ambayo ni simu janja maalumu kwaajili ya kuchezea magemu. Pia prosesa hii ina spidi ya 3.1GHz.

Prosesa za Simu janja

Picha: Muonekano wa Prosesa ya Snapdragon

Snapdragon 888; Prosesa hii ya simu janja ina spidi ya 2.84GHz na simu janja inayotumia prosesa hii ni pamoja na OnePlus 9.

SOMA PIA  Pokea na jibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia kompyuta

Exynos 2100; Kampuni ya Samsung inajihusisha pia na utengenezaji wa prosesa za simu janja na prosesa hizi huitwa Exynos. Aina hii ya prosesa inatumika katika simu janja ya Samsung Galaxy S21, Samsung Galaxy S21+ na Samsung Galaxy S21 Ultra. Pia prosesa hii ina spidi ya 2.9 GHz.

Endelea kutembelea tovuti yetu kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania