fbpx

Amazon kuunda programu ya kujipima nguo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya mauzo ya mitandaoni, Amazon inapanga kuunda programu ya kujipima mavazi kabla ya kununua japo si moja kwa moja itakayotumika kwenye simu janja.

Programu hiyo itahitaji kuwa na ufahamu wa mambo ya kimsingi ya mtu na itakagua picha za mteja kupitia mitandao ya kijamii kisha kupendekeza mavazi ambayo yanaweza kumfaa zaidi.

Baada ya ukaguzi huo, kampuni hiyo itapendekeza nguo ambazo mteja anaweza kufurahia. Aidha, itapendekeza mavazi ya mtu kulingana na eneo analoishi na kazi anayofanya.

Kwa kupitia picha za mteja, kampuni inaweza kuona wanachovaa, wanachoendesha na hata ndani ya nyumba zao ili kubashiri kitu ambacho mteja anawezakupenda sana kukinunua. Programu hiyo itakagua picha ili kubaini sehemu za mwili ambazo zitaunda taswira nzuri.

programu ya kujipima

Programu ya kujipima: Wateja wa Amazon watakuwa na fursa ya aidha kuzikubali ama kuzikataa; wateja wataweza kutafuta nguo zaidi ambazo programu imezipendekeza.

Programu hiyo sasa imeanza kuhofiwa kuwa huenda ikawa mwanzo wa mwisho wa biashara za ushonaji mitaani, mnamo Novemba 2018, utafiti ulionyesha kuwa biashara 2,692 za ushonaji zilifungwa kwa kipindi cha miezi sita. Vipi wewe una mtazamo gani kuhusu programu hiyo?

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Majaribio ya makazi ya kujazwa upepo ktk anga yafanikiwa! #Teknolojia
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.