Inasemakana kuna udukuzi mkubwa wa barua pepe umetokea katika mfumo wa huduma Microsoft Server Exchange, huduma ya barua pepe na kalenda ya Microsoft inayotumiwa na makampuni na mashirika mbalimbali duniani.

Kampuni hiyo na wadau wa usalama wa kidigitali wanarusha shutuma zao kwenda kwenye vikundi vidogo vya nchini China ambavyo vinapata msaada kutoka serikali na vyombo vya usalama vya nchi hiyo.
Hii ni moja kati ya udukuzi mkubwa kuwahi kufanyika, kwani huduma ya Microsoft Server Exchange inatumiwa na makampuni na mashirika mengi sana kwa ajili ya usimamiaji wa huduma muhimu za mawasiliano – barua pepe, kalenda.
Udukuzi huo unaweza ukawa umehusisha zaidi ya kompyuta-server 30,000 ila tayari Microsoft wametoa masasisho ya kuzuia udukuzi huo na inawasihi wateja wake kuruhusu masasisho hayo.
No Comment! Be the first one.