Zaidi ya wiki mbili tuliandika kuhusu mpango mpya ambao Twitter imetaka kuboresha kwa sababu kadha wa kadha ambapo sasa mpango huu umerudi nyuma kidogo.
Kupata ile alama ya pata kwenye akaunti ya Twitter si kazi ndogo hata kabisa kwani ni lazima upeleke maombi, yapitiwe na wahusika wakiridhia iwapo utakuwa umekidhi vigezo vyao basi utapewa kile ulichokiomba.
Hivi karibuni tulileta mbele ya macho yako wewe msomaji wetu habari kuhusu mpango mpya ambao Twitter imeuandaa kwa ajili ya kuweza kuidhisha akaunti ya Twitter mpango huo umerudishwa nyuma kidogo kutokana na changamoto zilizojitokeza.

Mei 20 mwaka huu Twitter iliruhusu watu kutuma maombi ya akaunti zao kuweza kuidhinishwa kwa huo mpango mpya na tangu hapo wapokea maombi mengi kiasi cha kwamba kufunga dirisha la kupokea maombi mapya.
Sababu ya kusitisha kupokea maombi ni kutokana na watu wengi kuomba akaunti zao kuidhinishwa sasa wahusika wameamua kufunga mlango kwa muda na kushughulikia walizozipokea na hatimae kutoa mrejesho kwa wahusika.
Je, wewe ni miongi mwa wale ambao walikuwa na mpango wa kupeleka maombi ya akaunti ya Twitter kuidhinishwa? Basi nikushauri tuu uwe mvumilivu tuu mpaka hapo watakaporuhusu kupokea maombi mengine.
Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.