Simu janja zimekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu kiasi kwamba tunazipendezesha na kuonekana nzuri zaidi kitu ambacho zinzifanya kuvutia kwa namna yoyote ile.
Kwa wale ambao tunapenda kubadilisha sura ya mbele kwenye rununu mniambie ni kwa kiasi gani kile ulichokiweka pale kinakufanya matumizi ya simu yaongezeke? Kabla hujanijibu fahamu hii OnePlus wamejinasibu na programu ambayo inabadilisha munekano kulingana na jinsi unavyotumia simu yako.
WellPaper ni programu tumishi ambayo inabadilika kila baada ya muda fulani kulingana na jinsi unavyotumia simu janja husika. Kwa lugha rahisi ni kwamba kuanzia sura ya mbele ahdi programu tumishi ulizozitumia mara kwa mara zinasogezwa karibu na kupangwa hivyo kufanya kuzifikia bila kuzunguka kuzifikia.
Programu tumishi-WellPaper inayojibadilisha muonekano kulingana na matumizi ya simu janja.
Habari kutoka OnePlus zinasema programu tumishi haichukui kiasi kikubwa cha chaji na inavyobadilisha muonekano hupanga vitu katika makundi sita yanayohusu: mitandao ya kijamii+mtindo wa maisha+muziki+mawasiliano, burudani+magemu+taarifa+biashara na vitu vingine.
Mfano wa mpangilio wa programu tumishi kwa usimaizi wa WellPaper.
WellPaper inafanya kazi ya kupanga kuanziakwenye muonekano ambao unajumuisha rangi hadi iddi ya programu tumishi ambazo zinatakiwa kukaa kulingana na matumizi ya mhusika. Halikadhalika, programu tumidhi inapatikana kwenye Playstore.
Vipi baada ya hapa utaenda kuishisha programu tumishi husika na kisha kufanya simu janja yako kuwa na muonakano wa tofauti?
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.