fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Mtandao Mtandao wa Kijamii Tovuti

Twitter waleta Stickers katika picha! #Apps

Twitter waleta Stickers katika picha! #Apps
Spread the love

Twitter wametangaza kuleta stickers katika picha ambazo zinatumwa katika mtandao wao maarufu wa kijamii. Watumiaji wataweza kuweka sticker katika picha zao ambazo wanasambaza katika mtandao huo.

twitter-stickers-feature-2.0

Picha kabla na baada ya kuwekewa sticker

Twitter sasa watawaruhusu watumiaji wao kutumia sticker katika picha zao wanazoposti katika mtandao huu kama vile ambavyo tumekwisha ona katika mtandao wa Snapchat. Hatua hii ya mtandao huu ni wazi inalenga kuongeza idadi ya picha ambazo zinasambazwa katika mtandao huu.

SOMA PIA  Fahamu Mambo Mapya Yanayokuja Kutoka WhatsApp

Inakadiriwa kwamba kuna walau picha milioni moja ambazo watu husambaza katika mtandao wa Twitter kila siku, idadi hii ya picha zinazo sambazwa katika mtandao huu pengine zitaongezeka hivi karibuni baada ya mtandao huu kuleta stickers katika picha.

twitter stickers

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika blogu ya Twitter uwezo wa kutumia stickers utakuja wiki chache zijazo baada toleo jipya la app hii kutoka kwa app za iOS na pia Android. Huduma hii itakuwa inapatikana katika sehemu ya picha ambayo tunaitumia kuedit picha, huduma hii pia itaenda katika toleo la Twitter.com ambalo linatumiwa zaidi na watumiaji wanaotumia kompyuta.

SOMA PIA  WhatsApp yaendelea kukimbiwa na waanzilishi wake; Pigo jingine kwa mmiliki wake

Pindi mtumiaji atakapotumia sticker fulani basi ataweza pia kuletewa picha mbali mbali ambazo zimewekewa stickers kama hiyo, huduma hii ya stickers kwa namna moja au nyingine hufanana na ile ya hashtag.

Je wewe ni mtumiaji wa Twitter? Umependezwa na jambo hili jipya?

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania